Monday, September 19, 2016

UTARATIBU WA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI KUTAMBUA BAJAJI NA BODABODA WAJA

 Image result for bajaji na bodaboda

Simu za mikononi sasa zitatumiwa na abiria wa Bodaboda na Bajaji kwa ajili ya kuboresha sekta ya usafiri huo pamoja na kupunguza vitendo vya uhalifu.

Akizungumza wakati wa kuzindua mkakati huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paulo Makonda amesema kuwa endapo itatokea jambo lolote,mtu atakuwa na uwezo wa kutumia simu yake ya mkononi kwa kuingiza namba maalum kama za huduma za kifedha na kwenda katika kipengele cha huduma ya Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Dar es salaam,kisha kuingiza namba iliyoko katika sare ya dereva.

Baada ya kuingiza namba hiyo ataweza kupatiwa jina halisi la dereva,namba ya usajili wa pikipiki yake,eneo lake analoegesha,kiongozi wa eneo lake kwa upande wa bodaboda na namba zake za simu pamoja na za kiongozi huyo.

Pia boda boda na madereva wa bajaji mkoani Dar es salaam,watakuwa na sare maalum ambazo watagawiwa bure pamoja na kofia ngumu.

Utaratibu huu utatekelezwa kwa kusajiliwa wamiliki na waendesha bodaboda na bajaji kwa namba maalum zitakazokuwa zimeandikwa katika sare watakazo kuwa wanavaa

Popular Posts

Labels