Wednesday, August 9, 2017

MFUMO MPYA WA ULIPAJI KODI YA PANGO LA ARDHI NCHINI.


 
      Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni.
 
Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli ya Serikali utakavyokuwa unatumika.
 Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.
Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.
Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi pia.
Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official serach), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.
Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini,

Monday, August 7, 2017

MAAMUZI TOKA KWA MKUTANO WA GAiN 2017 BRAZIL


 Image may contain: 30 people, people smiling, people standing, shoes and indoor

Mkutano Mkuu wa Mifumo ya utunzaji na usimamizi wa washiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni umemalizika katika jiji la Sao Paulo, Brazil Agosti 6 2017 ukiwa umefanya maazimio yafuatayo.

1. Taarifa rasmi na sahihi za idadi ya washiriki wa kanisa zitapatikana kupitia mfumo wa ACMS pekee.

2. Anwani za makanisa yote ya Waadventista zinapaswa zipatikane kupitia mfumo wa ACMS

3. Kila mwezi karani wa kanisa atatuma taarifa ya washiriki kwenda konferensi, ambayo itaendelea kutumwa mpaka ngazi ya juu.

4. Division ya Amerika kusini inajaribiwa na mfumo mpya wa 7ME ambao unaruhusu kila mshiriki kujaza takwimu zake mwenyewe na ukifanikiwa ndio utatumika rasmi ulimwenguni kote ifikapo mwaka 2018.

5. Idara zote za kanisa zitatumia mfumo wa ACMS kutoa taarifa za idara.

Mkutano huu ulikuwa na wajumbe 31 kutoka ulimwenguni kote na Divisheni ya Afrika Mashariki na kati iliwakiliswa na wajumbe wawili

Popular Posts

Labels