Monday, August 31, 2015

WATUMIAJI WA MITANDAO VIBAYA SHERIA KUWADHIBITI KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA MOSI



 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam leo.


Sheria mpya   ya Makosa ya Mtandao ya mwaka   2015 na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015 zitaanza kutumika rasmi kesho Septemba Mosi mwaka huu, hivyo watumiaji   na watoa huduma wameaswa kuzingatia sheria hizi ili kuepuka mkondo wa sheria.

 Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

“Sheria hizi ni nzuri zitaanza kutumika Septemba Mosi mwaka huu,kuanzia saa 6.00 usiku . zina maslahi katika nchi yetu. Ninatoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi salama ya mtandao kwa manufaa yako na maendeleo ya Taifa letu,” alisema Profesa Mbarawa.

 Aliongeza kuwa sheria hiyo ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 hazihitaji utungaji wa kanuni kwa kuwa iko wazi.

 Alisema tayari wizara imeanza kuelimisha watu kuhusu sheria hiyo na itendelea kuwajengea uwezo wadau mbalimbali.

Profesa Mbarawa alisema sheria ya makosa ya mtando ya mwaka 2015 na Tanzania sio nchi ya kwanza kuwa nayo, bali nchi mbalimbali zina sheria kama hiyo ,ambapo alitolea mfano Uingereza,India,Malaysia, Uganda na Korea ya Kusini.

 Akizungumzia kuhusu  madai sheria hiyo kuhusika na suala la Uchaguzi Mkuu, alisema si kweli, bali imekamilika katika kipindi hicho ndio maana baadhi ya watu wanadai hivyo.Aliongeza kwamba sheria hiyo imetunga ili kudhibiti matumizi ambayo  si mazuri. 

“ Mtu akitumiwa ujumbe akiupokea hapaswi kuisambaza  kwani atakapousambaza atakuwa na amefanya kosa,”alisisitiza.

Aliyataja baadhi ya makosa kuwa ni usiri, usalama wa upatikanaji wa taarifa za kompyuta na mifumo  kama vilekuingilia mawasiliano ya kompyuta au mifumo ya kompyuta kinyume cha sheria na wizi wa taarifa kimtandao.

Makosa  dhidi ya kompyuta ikiwa ni pamoja na,udanganyifu kwa kutumia kompyuta,kugushi kwa kutumia kompyuta wizi wa utambulisho wa mtu binafsi  mtandaoni, matumizi ya vifaa kinyume cha sheria.

Makosa yanayohusiana kimaudhui kama vile usambazaji wa ponografia, ponografia za watoto makosa dhidi ya ubaguzi wa rangi na chuki, michezo ya kmari mtanadaoni kiunyume cha sheria, kashfa na habari za uongo na makosa dhidi ya haki na hati miliki.

Pia inatambua muungano wa makosa inajumuisha kama vile utakatishaji wa fedha haramu na ugaidi kwa kutumia mtandao.

Kwa upande wa sheria ya miamala ya kieletroniki ya mwaka 2015, baadhi ya makosa likiwemo la wajibu wa watoa huduma kwa walaji, bidhaa ,huduma au mawasiliano ambayo hayajaombwa na uhalali wa Muamala wa elektroniki.

Aliongeza kuwa kanuni za sheria hiyo zinatayarishwa zikiwa tayari zitangazwa  na zitaanza kutumika wakati wowote.
chanzo:daresalaam-yetu.blogspot.com

Saturday, August 29, 2015

ALIYEWAHI KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA APPLE AZINDUA AINA MBILI ZA SIMU ZA ANDROID


Feeling Good Feeling Good




John Sculley aliyewahi kuongoza kampuni ya Apple kwa muda wa miaka 10 (muongo mmoja) tangu mwaka 1983 amezindua simu yake ya kisasa ya Obi Worldphone ambayo inatarajiwa kufanya vyema sokoni hivi sasa na inatarajiwa kuwa sokoni rasmi hivi karibuni.



Simu hii iko katika muundo wa aina mbili SF1 na SJ1.5

Aina ya simu hizi zimeundwa kwa ushirikiano na studio ya ubunifu ya Ammunition iliyoko San Francisco,Marekani  iliyoanzishwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa ubunifu wa kampuni ya Apple Robert Brunner.



Simu hizo zilizounda kwa mfumo endeshi wa Android  5.1 zinateknolojia ya kutumia simcard mbili zenye uwezo wa 4G

Designed to exceed expectations
SF1
Ina  64-bit Snapdragon 615 processor  ina uwezo wa 32 GB yenye RAM ya 3GB huku ikiuzwa kwa dola 249 au yenye 16 GB na RAM ya 2 GB ikiuzwa dola za kimarekani 199 na ikiwa na slot ya kuweka microSD kuanzia uwezo mdogo hadi GB 64.

SFI ina kamera ya nyuma yenye uwezo wa -megapixel 13 inaweza kupiga picha bila kutoa mwanga ama kutoa mwanga wakati kamera ya mbele ina megapixel 5




For living
SJ1.5


Hii ni ndogo kuliko ile ya SF1 ina urefu wa nchi tano ina prosesa ya 1.3 GHz
Ina memory ya ndani ya 16 GB na RAM ya 1GB  na slot and supports microSD kuanzia ya chini kabisa mpaka  32GB. Kamera ya nyuma inauwezo wa  kupiga picha kwa megapixel 8 na kamera ya mbele megapixel 5.
Obi Worldphone sio jina la biashara la kampuni jipya bali lilianza mwaka 2014 kwa kutumia jina la Obi Mobiles ambapo ilijaribu kuuza simu zilizoundwa toka China na kuuzwa huko India na Uarabuni.
Ukosefu wa kutofautisha na uhafifu wa ubora wa matoleo ya simu hizo walifunga biashara ya simu huko India mapema mwaka huu.

Simu hizo zitakazokuwa katika mwonekano wa  aina mbili tofauti na zenye rangi nyekundu,nyeupe na nyeusi zinalenga kuwavutia vijana katika nchi za   Asia, Afrika na Mashariki ya Kati.
Simu za Obi zitaanza kupatikana mwezi Oktoba katika nchi za Vietnam, Indonesia, Thailand, Umoja wa Nchi za Kiarabu, Saudi Arabia, Kenya, Nigeria, Tanzania, Afrika Kusini, Pakistan, Uturuki na  India.
Watafiti wa masoko ya simu wanaeleza kuwa itakuwa jambo la kuvutia kuona simu hizo za Obi zikiingia kwenye ushindani katika nchi za Asia na Afrika ukilinganisha na kupotea kwa simu za Xiaomi, Honor na  Motorola katika miaka iliyopita japo wanahofu kuwa simu za Obi nazo zaweza zisifanye vyema kwenye soko la ushindani wa simu za mikononi katika maeneo hayo.



.Angalia video hizi.


Thursday, August 27, 2015

MAWASILIANO YA INTANETI KWA SIMU YAZUIWA KATIKA MJI WA AHMEDABAD NCHINI INDIA

A slice of Ahmedabad. Gujarat is home to India's current Prime Minister Narendra Modi
Sehemu ya mji wa Gujarat  ambako anatoka Waziri Mkuu wa sasa wa  India Narendra Mod
Huduma za mawasiliano ya intaneti kwa njia ya simu zimezuiwa katika jimbo la Gujarat lenye wakazi karibu milioni 63  nchini India kutokana na ghasia za  wapinzani wa jumuia ya Patel baada ya mmoja wa wafuasi wake kukamatwa na polisi katika mji wa Ahmedabad wenye wakazi wapatao milioni 3.5 kwa mujibu wa sensa ya umoja wa mataifa ya mwaka 2001

Jamii ya Patel walituma ujumbe mfupi wa maneno kwa raia kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kutosababisha machafuko katika eneo hilo.
Ujumbe huo umekuwa ukiambatanishwa na  picha za video na sauti kupitia mtandao huo

Afisa mmoja wa Polisi amesema kuwa walikuwa wakifuatilia taarifa kuwa watu wamekuwa wakiwasiliana kuhusu suala hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp ingawa ametoa taarifa kuwa huduma za intaneti zitarejea baada ya kuwa wamejiridhisha na hali ya utulivu kama kawaida katika eneo hilo.
Taarifa zingine zinaeleza kuwa mawasiliano ya intaneti kwa njia ya simu yamezuiwa katika jimbo lote la Gujarat.

Wednesday, August 26, 2015

KAMPUNI YA TIGO YAJA NA KAMPENI YA CHAGUA TIGO PESA


 Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi katika uzinduzi wa kampeni ya  Chagua Tigo Pesa, Inalipa. Kulia ni Meneja  Chapa wa Tigo, William Mpinga.
 Meneja  Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Kampuni ya simu ya mkononi ya tigo Tanzania imezindua Kampeni iitwayo"chagua tigo pesa,inalipa"ikiwa na lengo na la kuongeza upatikanaji wa fedha kwa njia ya simu ya mkononi kwa wateja.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Ruan Swanepoel alisema huduma hiyo ikiwa na muonekano mpya na sura kwa wateja wake wanaotumia huduma ya tigo pesa Tanzania nzima.

Alisema kuwa kwasasa mtandao wa tigo umeenea kwa wingi hapa nchini na unatumiwa na asilimia 90 ya wananchi wote wanaomiliki simu za mkononi.

Alisema kuwa mtandao wa tigo unakikisha inatoa huduma stahiki kwa wateja wakena kuhakikisha huduma ya tigo pesa inazidi kuwa na huduma pendwa kwa sababuinapatikana kirahisi na makini.

Alisema kuwa huduma hii inalipa kwa wateja wake na kukopa fedha hasa kwa wale wenye kipato kidogo na wasio na huduma za kibenki.

Alifafanua kuwa wateja wa tigo pesa watanufaika na kampeni hii kwa kuypata vifurushi vya bure kila wannunuapo bidhaa na kulipia kwa tigo pesa kutoka kwa wauzaji waliosajiliwa.

Pia aliongeza na kusema kuwa wateja watapata riba kila baada ya miezi mitatu kulingana na kiasi cha fedha ya kifurushi ambacho mteja atamnunulia mtu mwingine kwa tigo pesa.
chanzo: mtandao wa www. habari za jamii.com


Monday, August 24, 2015

KUTOKA FACEBOOK NA TWITTER HII LEO




Thursday, August 20, 2015

GOOGLE WAZINDUA SIMU YA KISASA YA BEI RAHISI KWA AJILI YA AFRIKA



Google imezindua simu ya kisasa ya bei rahisi barani Afrika. 

Simu hiyo, Hot 2 ambayo haina 'makorokoro' mengi itaanza kupatikana katika nchi sita za Afrika. 

Itagharimu kati ya dola 85 na 100. Licha ya kuwa si watu wengi watakuwa na uwezo wa kuinunua, lakini ni bei rahisi kulinganisha na iPhone ambayo inauzwa hadi dola 1,000.

 Uzinduzi huu ni juhudi za Google kujaribu kulikamata soko linalokua kwa kasi la simu za kisasa, ambapo watumiaji wengi bado hawana uwezo wa kuwa na vifaa vinavyoweza kuuganishwa kwenye mtandao wa internet.

Hot 2 imeshaanza kuuzwa na baadhi ya wafanyabiashara wa Nigeria na pia inapatikana kwa kununua kwenye mtandao kwa kiasi cha Pesa za Nigeria Naira 17,500 sawa na dola 88 na itapatikana pia hivi karibuni katika nchi za Ghana, Ivory Coast, Kenya,Misri na Morocco. 

Kwa mujibu wa Google takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya wanaigeria milioni 50 wanaotumia intaneti asilimia 95 kati yao wanatumia simu za mikononi.

Simu hiyo ambayo ipo katika rangi nyeusi,,nyekundu,nyeupe,dhahabu na blue ina prosesa ya quad-core MediaTek yenye memory ya 16GB na inauwezo wa kutumiwa na sim card mbili,ikiwa imeundwa kwa program endeshi ya Android 6.0 Marshmallow 

 

Saturday, August 15, 2015

WAZIRI ATOA ELIMU YA SHERIA YA MITANDAO KWA JESHI LA POLISI NCHINI TANZANIA

Serikali ya Tanzania imesema shilingi trioni 54.4 zitakuwepo kwenye hatari ya kuingia katika mikono ya wahalifu wa mitandao,endapo Sheria za Mitandao na Miamala ya fedha haitatumika.

Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa ametoa hadhali hiyo wakati akifungua mafunzo ya viongozi wa Jeshi la Polisi yaliyolenga kuwapa elimu kuhusu utekelezaji wa sheria hizo kabla ya kuanza kutumika Septemba Mosi mwaka huu.

Amesema fedha hizo sawa na trioni 4.4 kila mwezi ,watu wanahifadhi na kutumia kupitia miamala mbalimbali ya mitandao ya simu za mikononi.

Profesa Mbarawa amesema fedha hizo lazima zilindwe kwa kuwekewa sheria zenye kuzuia na kutoa adhabu kwa watu watakaoingilia mihamala ya fedha.

Friday, August 14, 2015

USALAMA MITANDAO: TANZANIA INA CHA KUJIFUNZA KUTOKA KENYA.

 
Nimekamilisha vikao vya usalama mitandao vilivyofanyikia jijini Nairobi kufuatia mualiko maalum nilioupata. Katika vikao hivyo niliwasilisha mada mbili (ya kwanza ikiwa ni namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao na mada ya pili ikiwa ni namna ya uchunguzi wa makosa ya digitali kitaalam) katika mada hizo mbili ambazo zilipokelewa vizuri na kupelekea mijadala ya kipekee kuna mengi  nikajifunza kutoka kwa washiriki. Aidha, nilishiriki mijadala duara iliyojikita katika changamototo mbali mbali za uhalifu mitandao na kuiangazia sharia mtandao ya nchi ya Kenya.

Kenya ni miongoni mwa nchi tatu barani afrika ambazo zimeorodheshwa kuwa na uhalifu mkubwa sana wa kimtandao nyingine ni Nigeria pamoja na Afrika ya Kusini. Tukijadili takwimu za kutisha duniani kote, tulishuka na kuangazia bara la Afrika na baadaye Afrika Mashariki na hatimae kujikita na twakwimu za nchi ya Kenya.

Kwa upande wa Kenya kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa katika mkutano, hadi kufikia Mwezi wa saba mwaka huu (2015) kuna simu 34.8 Milioni  huku watumiaji wakiwa ni 26.0 Milioni. Aidha, matumizi ya intaneti ni 29.1 milioni ambayo ni sawa na 65% “penetration”. Takwimu hizo zinasindikizwa na upotevu wa dola za kimarekani 20 milioni ($20 Mil) kila mwaka kutokana na uhalifu mtandao.

Palizungumzwa matukio ya kudukuliwa kwa tovuti nchini humo ambapo, tovuti za serikali 103 ziliathiriwa mwaka 2013, na 3 kwa mwaka wa 2014 huku twitter ya serikali mwaka jana (2014) ikiwa ni miongoni mwa zilizo dukuliwa na kutumiwa vibaya. Nilihoji tofauti kubwa ya udukuzi wa tovuti na kujulishwa baada ya tukio la aina yake la mwaka 2013 serikali iliamua kuzifunga tuvuti zake nyingi hasa zile zilizo onekana hazina umuhimu sana kua hewani kitu ambacho kilichangia kupunguza namba kubwa ya udukuzi kwa mwaka 2014.

Kwa upande wa pesa zinazopotea kwa nyia ya simu – Miamala inayofanywa kwa njia ya simu ni asilimia kumi (10%) ya fedha za miamala yote kila mwezi huku idadi hiyo kuonekana kushtusha wengi.

Ikumbukwe nchi ya Kenya, matumizi mabaya ya mitandao yalisababisha kuchochea na kutokea vurugu zilizosababisha matatizo makubwa sana kipindi cha uchaguzi kilichopita ambapo kwa mujibu wa mchambuzi mmoja wa maswala ya uchanguzi alichapisha andiko na kueleza mitandao ilikua chanzo kikubwa cha kueneza chuki na fujo kipindi cha uchaguzi uliopita.


Yote hayo – Takwimu zote hizi kwa nchi ya Kenya zimesababishwa na jambo moja zuri sana ambapo ni kua na uwazi wa takwimu na taarifa za kihalifu mtandao ambapo kwa Afrika imekua ni nchi pekee iliyofanikisha swala hili. Itakumbukwa nilitoa pongezi kwa nchi hiyo baada ya ku ainisha takwimu zake kwa mara ya kwanza mwaka jana (2014) na kufanya iwe ya kwanza Afrika katika hili.

Kilicho nifurahisha zaidi ni hatua taifa hilo limechukua kukabiliana na uhalifu mtandao. Tayari nchi hiyo ina “National cybersecurity master plan” na sheria mtandao ambapo kosa la udukuzi adhabu ni miaka kumi (10) jela, faini ya KSH 10,000 au vyote kwa pamoja. Pia ina strategy ya maswala ya usalama mitandao na kupitia mamlaka ya TEHAMA “ICT Commission” wamesha zindua andiko linalotoa muongozo wa kuwalinda watoto katika mitandao.

Hayo ni uchache katika mengi ambayo tayari taifa limeweka katika mikakati yake. Zaidi ni mikakati ya kukuza uelewa na ujuzi kwa watu wake ili kuweza kuendelea kutumia vizuri mitandao pamoja na namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao.Aidha, Mpango wa serikali kuimarisha ushirikiano ambapo CERT – KENYA inajumuisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama huku mashirika binafsi yakiwa na nafasi kubwa kuisaidia ili kukabiliana na uhalifu mtandao. Mfano wa Hili ni mshiriki kutoka Microsoft alipo tolea ufafanuzi kampuni hiyo inavyo fanya kazi karibu na serikali ya kenya kukabiliana na uhalifu mtandao nchini humo kupitia CERT –KENYA.

Kilicho nipa faraja kubwa ni kauli ya pamoja kua Kenya imefanya mengi lakini pakakubalika kua kuna mengi bado yakufanyia kazi ili kuweza kupiga hatua zaidi katika maswala ya usalama mitandao nchini humo. Ni marachache sana mataifa yanakiri kua bado safari ni ndefu ili kufikia malengo. Pamoja na hatua kubwa nilizo ziona katika nchi hiyo lakini bado walikiri kuna safari ya kupiga ili kusonga mbele zaidi.

Tulipata kuangazia aina za uhalifu na namna zinavyofanyika kwa nchi ya kenya – hakika aina hizi hapa kwetu pia ziko njiani na hofu yangu kubwa ni kwa kiasi gani tutakua tumejiandaa? Kujua tatizo nihatua za awali za utatuzi na wengine wakinyolewa ni vizuri tukatia nywele maji.

Kwa ufupi mambo yakufanyiwa kazi ambayo bado ni changamoto kwa mataifa yote yaliyoweza kujadiliwa ni pamoja na:-

Bado kumekua na dhana kua swala la usalama mitandao ni la kundi fulani ( wana TEHAMA – waliojikita katika maswla ya usalama mitandao) Hili sasa linatakiwa libadilike na katika kila kampuni au serikali lazima swala hili lianzie katika ngazi ya juu kushuka hadi ngazi ya mmoja mmoja (Kila mtu)

Bado udukuzi na uhalifu mtandao kwa ujumla umeendelea kushika kasi huku ugunduzi wa tukio kutokea kuchukua hadi siku 200 kwa wastani baada ya tukio ambapo tumekubaliana kimsingi hii ni namba kubwa sana na kunakila sababu ya kushusha namba hizi – pia kuwe na njia za kuzuia tatizo kabla halijatokea ambazo ni madhubuti kwa kufanyia kazi ushauri unaotolewa wataalam.

Uhalifu wa ndani (Insider threats) bado ni changamoto kubwa sana katika anga ya dunia na imeonekana kusahauliwa kabisa huku jitihada za dhati zikianza kuonekana kukuza uelewa kwenye hili na sasa tayari “Mr. Robot” tamthilia mpya ya kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao imejikita kwenye hili.

Uhaba wa wataalam katika maswala ya usalama mitandao ni la kuchukuliwa hatua za haraka kwa kuhimiza mitaala ya usalama mitandao kuingizwa vyuoni huku wataalam wanaopatikana kutumika vizuri – Wenye ujuzi watumike mahali husika kwani imeonekana bado kuna changaoto ya kutotumiwa vizuri wataalm wa maswala haya inaypelekea uhalikfu kukua kwa kasi kila kukicha. Hili limeonekana zaidi barani Afrika na mataifa kadhaa wamesha anza kulifanyia kazi ili kuweka mabo sawa.

Sheria mitandao kutumiwa ipasavyo lakini pia iambatane na kua na waelewa wa uchunguzi wa makosa haya kwa kuzingatia maadili na taratibu za kitaalm zilizo sahihi na kuhakiki uelewa unasambazwa kwa watu ili kuepusha wimbi kubwa la wahalifu mtandao wanao fanya uhalifu huu bila kujua kuingia matatani – Imeonekana bado kuna ugumu mkubwa wa kesi za uhalifu mtandao kuvuka mahakamani na watuhumiwa kuwajibishwa kutokana na udhaifu mkubwa kwa mataifa ya Afrika mashariki walionao katika kufata taratibu za kuwasilisha kesi hizi ipasavyo mahakamani (Ujuzi bado Uko chini sana).

Ushirikiano wa ndani ya mataifa pamoja na kuvuka mipaka bado ni changamoto inayo onekana kuzikumba Nchi nyingi hasa barani Afrika huku Kenya ikiwa imeliona hili na imepiga hatua nzuri kwa ndani ila bado wanakiri kuvuka mipaka bado ni changamoto kutokana na utayari wa mataifa mengine katika hili.

Hayo ni kwauchache tu kwani mengi sana yamejadiliwa na nategemea kutumia muda wangu kadhaa kuwasilisha kidogo kidogo ili tuweze kuendelea kujifunza zaidi kupitia vyanzo mbali mbali vya habari.
NA:Yusuph Kileo

Tuesday, August 11, 2015

SHERIA YA MAKOSA YA UHALIFU WA MITANDAO NCHINI TANZANIA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA MOSI MWAKA 2015



Wananchi wanaotumia vibaya mitandao huenda wakajikuta matatani hivi karibu kwani Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuwa  ifikapo Septemba mosi, mwaka huu, Sheria ya Uhalifu wa Mitandao itaanza kutumika humo.

Akizungumza na   waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy amekiri kuwa pamoja na kwamba mamlaka hiyo imefanya kazi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya utumiaji sahihi wa mitandao hiyo, bado matumizi yake si mazuri hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Aidha Mamlaka hiyo imebainisha kuwa kwa sasa Tanzania inaongoza kwa kuwa na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, jambo linalosababisha taarifa za mitandao mingi kutoaminika hadi nchi za nje kutokana na kujaa uzushi, uongo, lugha za uchochezi na picha za matusi.

Amesema kutokana na kukithiri kwa matumizi mabaya ya mitandao nchini, kwa sasa nchi nyingi haziamini tena taarifa za mitandao ya kijamii na wala hawazitumii hali inayopaswa kubadilishwa.

Mungy amesema mamlaka hiyo kazi yake kubwa ni kusimamia matumizi ya mitandao hivyo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, itahakikisha inadhibiti kwa kuelimisha na kuwabaini wale wote wanaotumia vibaya mitandao hiyo.

Popular Posts

Labels