Friday, January 31, 2014

MAKAMPUNI YA MITANDAO YA SIMU NCHINI MAREKANI KUFANYA UTAFITI WA NAMBA ZA SIMU KUWA IP

A cell tower stands alone in the desert

Natumaini umeshawahi kusikia ama unafahamu kuhusu teknolojia ya kusafirisha mawimbi ya sauti kwa njia ya intaneti ( VoIP) ambayo si teknolojia mpya.

Kamisheni ya Shirikisho la Mawasiliano (FCC) ambayo ni wakala wa serikali ya  Marekani inayahimiza makampuni ya mitando ya simu kufanya utafiti iwapo namba za simu zinaweza kuwa IP ambapo hata katika namba za dhalula ambazo hutumiwa bure kwa huduma za haraka zitumike kuwasiliana kwa kutumia tovuti.

IP ni namba ya pekee ambayo hutumika katika utambuzi wa komputa ama kifaa cha mawasiliano kilichopo katika mtandao ili kiweze kuwasiliana na komputa ama kifaa kingine.

Tovuti ya engadget na shirika la habari la Reuters zimeikariri  FCC  karibuni  ikieleza kuwa makampuni ya mitandao ya simu ambayo yanataka kushiriki kwenye utafiti huyo yanapaswa kuwasilisha mawazo yao kuhusu jambo hilo mwishoni mwa  mwezi februari mwaka huu na maamuzi ya jambo hilo yanatarajiwa kutolewa mwezi machi mwaka huu.

Tuesday, January 28, 2014

RAIS KIKWETE APOKEA TABITI 61 ZA SHULE YA SEKONDARI YA WAMA NAKAYAMA


  • Serikali kusambaza tabiti za kufundishia sekondari
  • Yaanza kazi hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya Marekani ya Opportunity Education Trust

Serikali inakusudia kutoa maelfu kwa maelfu ya tabuleti za kufundishia masomo mbali mbali  kwa wanafunzi na walimu wa shule za sekondari nchini kama njia ya ubunifu zaidi, ya kisayansi na ya uhakika ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

Ili kufanikisha mpango huo, Serikali inakusudia kuingia ushirikiano (partnership) na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Opportunity Education Trust ya Marekani ambayo , Jumatatu, Januari 27, 2014, ilitarajia kuzindua mpango wa majaribio wa utoaji wa tabiti hizo kwa wanafunzi na walimu wao wa shule za sekondari nchini.


Mpango wa Serikali wa kusambaza tabiti kwa wanafunzi na walimu wa shule za sekondari ulitangazwa usiku wa, Jumapili, Januari 26, 2013 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokutana na kuzungumza na Bwana Joe Ricketts, mwenye taasisi ya Opportunity Education Trust na mmoja wa matajiri wa Marekani.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amemweleza kwa undani Bwana Ricketts hatua ambazo zimechukuliwa na Serikali yake kupania na kuboresha elimu tokea mwaka 2006, hatua ambazo zimechangia kupanua kwa kasi na kwa kiwango kikubwa wigo wa utoaji elimu nchini na changamoto ambazo zimezuka kutokana na upanuzi huo mkubwa.

Rais Kikwete amesema baadhi ya changamoto hizi ni ukosefu wa walimu, na hasa walimu wa masomo ya sayansi, na ukosefu wa vitabu vya kufundishia changamoto mbili kubwa ambazo zinatatuliwa na matumizi ya tabuleti.

“Mbali na upanuzi mkubwa wa nafasi za wanafunzi kupata elimu ya ngazi mbali mbali, pia tumepanua sana ufundishaji wa walimu. Mwaka 2005, vyuo vyetu vyote vilikuwa vinatoa walimu 500 sasa tunatoa walimu 12,000 kwa mwaka. Hivyo, tunaamini kuwa katika mwaka mmoja ama miwili ijayo, tutakuwa tumemaliza tatizo la walimu wa masomo ya sanaa,” Rais Kikwete alimwambia Ricketts na kuongeza:

“Lakini bado tunakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi, kama zilivyo nchi nyingine. Tuna upungufu wa walimu 26,000 na kwa mwaka vyuo vyetu vyote vinahitimisha walimu 2,100 tu. Hii ina maana kuwa itabidi kusubiri miaka 13 kuweza kumaliza tatizo hili kwa mahitaji ya sasa. Hili haliwezekani na hii ndiyo maana halisi ya kutumia sayansi na teknolojia ya namna hii kufundishia wanafunzi wetu.”

Rais Kikwete alisema kuwa matumizi ya teknolojia kufundishia nchini ni jambo linalowezekana kwa urahisi kwa sababu mtandao wa mawasiliano wa National Fibre Network ambao karibu umefikia kila wilaya sasa.

Rais Kikwete alimshukuru Bwana Ricketts na  taasisi yake kwa kukubali kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu nchini kwa kusambaza teknolojia ya kisasa kama moja ya njia za ubunifu zaidi za kufundishia hasa masomo ya sayansi.

Chini ya mpango huo wa majaribio wa kusambaza teknolojia hiyo ya kisasa, taasisi ya Opportunity Education Trust inatoa tabuleti 1100 kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa sekondari katika shule 33.

Bwana Ricketts ambaye ni mwenyeji wa Omaha, Nebraska alimwambia Rais Kikwete: “Hapa tunafanya majaribio na Tanzania ni nchi ya kwanza duniani miongoni mwa nchi ambazo tunaunga mkono mipango ya maendeleo kunufaika na mpango huo wa majaribio. Ni azma yetu kuwa baada ya kuwa tumefanya tathmini ya mafanikio na changamoto za hatua hii ya majaribio, tutaupanua mpango huu kushirikisha shule nyingi zaidi kwa kushirikiana na Serikali kwenye mpango wake mkubwa wa kusambaza teknolojia hii katika shule zote za sekondari hapa Tanzania.”

Bwana Ricketts na wataalam wake pamoja na maofisa wa Serikali wameanza kutekeleza mpango huo, Jumatatu, Januari 27, 2014, kwa kutoa tabiti kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wama Nakayama iliyoko Mkoa wa Pwani.
Shughuli hiyo itahamia Zanzibar na Pemba, kabla ya Bwana Ricketts na wataalam wake kutoa tabiti kwa shule zilizoko mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Kagera na Morogoro.

Shule zinazonufaika katika mpango huo ni za Serikali na binafsi na kwa kuanzia masomo ambayo yanapatikana katika tabiti hizo ni hesabu, jiografia, historia na kiingereza.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

27 January, 2014

IFAHAMU KADI YA MANUNUZI YA B-PESA

 

 

Kadi ya B-PESA iliyoanzishwa kutumika nchini Tanzania na Smart Banking Solutions LTD kadi ya kielektroniki kwa ajili ya malipo,kuhamisha na kusimamia fedha.

Ni kadi ya malipo ya kabla,kwa urahisi ,wepesi, usalama na haraka na kuondoa kuwa na pesa taslimu wakati wa mahitaji ya matumizi ya fedha.

Kwa mujibu wa Maofisa wa Smart Banking Solutions LTD, Robert Boniface na Elibariki Lukumay walipoitambulisha kadi ya manunuzi ya B-Pesa katika kipindi cha Maisha na Teknohama cha Morning Star Radio jijini Dar es salaam wameeleza kuwa kadi ya B-PESA inapatikana sehemu yoyote iliyooneshwa alama ya B-PESA na inajumuisha benki wanachama,mawakala na maduka ya kadi hiyo nchini Tanzania.

Kusajili kadi ya B-PESA ni kufika kwa wakala ukiwa na simu yako ya mkononi,ukimaliza kujisajili utapokea ujumbe mfupi wa simu ambayo inathibitisha usajili wako na namba yako ya siri ambapo itakuwa tayali kutumika.

Maofisa hao wanaeleza kuwa faida ya kuwa na kadi hii yenye hadhi ya kibenki ni kwamba haulazimiki kubeba fedha taslimu,usalama wa pesa kwa kuwa inatumia teknolojia ya kisasa yenye ubora wa kudhibiti na kulinda namba ya siri,kadi hiyo haijaunganishwa na akaunti ya benki ya mhusika na ukiwa na kadi ya B-PESA unaweza kuitumia kwa wakala yoyote wa kadi hiyo kutoa pesa,kulipia bili na kuhamisha fedha kwenda kadi nyingine ya B-PESA.
Kadi hiyo pia imeunganishwa na tovuti ya www.bpesa.com 

Thursday, January 23, 2014

PAPA ASEMA INTANETI NI ZAWADI KWA DUNIA NZIMA

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa Internet ni zawadi kwa dunia nzima kutoka kwa Mungu lakini akaonya kuwa matamanio ya kutaka kuwasiliana zaidi kutumia Intaneti kunawatenga watu kutoka kwa familia na marafiki zao.

Amewataka waumuni wa kikatoliki kujiunga na mfumo wa dijitali. "Intaneti... inatoa nafasi ya mafanikio mengi. Hiki ni kitu kizuri bila shaka ni zawadi kutoka kwa Mungu,'' alisema Papa.

Katika ujumbe wake kwa dunia nzima ambao hutolewa kila mwaka, Papa amesema kuwa mfumo wa dijitali, unapaswa kuwa mtandao wa watu wala sio nyaya tupu.

Papa mwenyewe ana akaunti kwenye Twitter ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni kumi.

Amehimiza kuwa mawasiliano yanapaswa kuhusisha hisia na mawazo, watu kukutana na kujuliana hali.

Kadhalika amewataka waumini wa kikatoliki kutodhani kuwa ni mawazo yao na imani zao pekee ambazo ni muhimu wakati wakiwasiliana na watu wa dini nyinginezo.

Chanzo:BBC

Wednesday, January 22, 2014

TUZO ZA NJIA ZA MAWASILIANO ZA KIDIJITALI KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM MWAKA HUU



 TANZANIA DIGITAL MEDIA AWARD (TDMA)

Opt Media Information Solutions kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hapa Tanzania, inakuleteeni Tunzo za Njia za Mawasiliano za Kidijitali, zijulikanazo kama “Tanzania Digital Media Awards” (TDMA)



"Tanzania Digital Media Awards " ( TDMA ) inalenga kusherehekea na kutambua uvumbuzi unaotumia Wavuti, Tovuti, na Mitandao ya Kijamii katika kutoa huduma bora kwa wateja hasa kwa kutumia mawasiliano ya digitali kwa makampuni na mashirika mbalimbali hapa Tanzania.

TDMA, mradi unaosimamiwa na Opt Media Information Solutions (OMIS ), mnano Aprili, 2014, jijini Dar es Salaam, tutakuwa na tukio la sherehe za tunzo za utoaji tunzo zitakazo kusherehekea uvumbuzi na ubora katika mawasiliano ya kidigitali ya kisasa na yale ya kawaida yanayotumiwa na makampuni na mashirika mbalimbali ndani ya Tanzania, ili kuwafikia wateja au wadau wao. Toleo hili la Tunzo pia litatoa tuzo maalum za heshima na kutambua watu maarufu na wa kawaida wanaotumia teknologia za mawasiliano kuleta mabadiliko chanya katika jamii, ama wale wanaotengeneza teknologia zilizo na manufaa kwa jamii.

Ili kuhakikisha kwamba tunzo hizi zinapata heshima na sifa chanya kutoka kwa wadau na umma kwa ujumla, washindi wa tuzo watapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na umma pamoja na zile zinakazopigwa na jopo la majaji waliona mapenzi, shauku, utaalamu na watumiaji wa njia hizi za mawasiliano ya kidigitali hapa Tanzania, kutoka katika taasisi mahususi za umma na binafsi – yaani watalamu wa TEKNOHAMA, waandishi wa habari, watu wa masoko na mawasiliano pamoja na upashaji habari.


Katika siku za nyuma ikumbukwe kuwa, tovuti ilikuwa chombo cha kawaida tu ili kufanya wamiliki wake wawe mtandaoni, lakini hili miaka ya karibuni limebadilika. Kwani leo watumiaji ama  wasomaji wa tovuti wamebadilika zaidi. Pia mageuzi katika mawasiliano kwa kutumia mitandao ya kijamii yameleta mtazamo mpya katika tasnia ya ‘mawasiliano ya kisasa’ katika biashara, serikali, na asasi za kiraia. Kwa pamoja, mtandao, na mageuzi ya teknologia ya simu za mkononi imefanya watumiaji wa mitandao na wasiliano ya dijitali wadai uzoefu wa kudumu na tija kutokana na mawasiliano ya makampuni na mashirika mbalimbali kwa wadau wao. Kwa minajili hiyo unaweza kuona jinsi mawasiliano ya kisasa yalivyoleta mafanikio makubwa kwa mawasiliano ya makampuni, mashirika na asasi za kiraia. Hivyo katika zama hizi bidhaa si tena ile ambayo tunawaambia walaji kuwa ilivyo...bali bidhaa ile ambayo wateja wanaambiana jinsi wanavyoiona kwa mitazamo yao. Hiyo ndiyo nguvu mpya ya mawasiliano digitali na mitandao ya kijamii.

Tunzo za “Tanzania Digital Media Awards” zitafanyika katika moja ya hoteli za nyota 5 hapa Dar es Salaam, Aprili hii ya mwaka 2014. Taarifa zaidi juu ya mgeni rasmi na wa heshima, ukumbi pamoja na tarehe kamili zitatolewa katika mkutano wa waandishi wa habari ambao utafanyika Februari 28, 2014 hapa Dar es Salaam.


Ombi letu kwa umma na wadau wenye kutakia mafanikio ya Tunzo za TDMA, ni kuwa sote tunatambua umuhimu, na matumizi ya mawasiliano ya kidijitali kama mitandao ya kijamii, tovuti, wavuti nk kama sehemu muhimu ya kufanikisha mawaliano ya makampuni, mashirika na serikali. Tuendelee kutumia mawasiliano haya kwa tija na weredi kwani habari na wasiliano ni muhimu kwa kila mtu, kila kampuni , serikali, na mashirika, hivyo tuizitegemeze Tunzo hizi za Chaguo la Watu.


Ahadi yetu kwa umma ni kuwa tukio hili litaendelea kufanyika katika miaka ijayo na litakuwa ndiyo tukio kubwa litakalo kutanisha watu wakaliba mbalimbali wa ulimwengu wa biashara na mashirika. Pia lengo letu ni kuhakikisha viwango vya juu ambavyo ndio msingi wamafanikio ya Tunzo hizi unafuatwa ili kulinda heshima na taswira za wadau na wafadhili wetu kwa kuwalete usiku wa sherehe zilizoandaliwa kwa uweredi mkubwa.



IMETOLEWA NA:



JONATHAN N. MNYELA

GENERAL MANAGER

OPT MEDIA INFORMATION SOLUTIONS



+255714060608

Saturday, January 18, 2014

FAHAMU NAMNA AMBAVYO SIMU YAKO INAVYOWAFAHAMISHA WENGINE MAHALI ULIPO



 
 
Miongoni mwa mambo ambayo simu yako ya kisasa  inaweza kuyafanya ni kukufahamisha ilipo kuliko kompyuta yako ya mezani,kompyuta mpakato wakati mwingine hata tabiti ambavyo wakati mwingine ni vigumu kuwa navyo muda wote,simu za kisasa inaweza kujumuisha eneo ilipo na data katika upatikanaji wa habari ama taarifa  mbalimbali.

Kama ilivyo katika masuala mbalimbali ya teknolojia za kidijitali uwezo huu wa simu una uzuri wake na ubaya wake.Watumiaji wa simu wamekuwa wakijiuliza kuhusu masuala ya faragha hasa linapokuja suala la kufahamu mtumiaji wa simu alipo katika usalama wake.
Pia watu wengine hawako makini nahawafahamu  ni teknojia  gani ya kutambua mahali walipo na hasa kutokana na ukweli kwamba kuna program tumishi nyingi ambazo huhitaji kuonesha mahali mtumiaji wa simu alipo.

1.GPS
Global Positioning Systeam ni mtambo wa satellite unaotambua na kuelekeza maeneo mbalimbali hapa duniani.Mtambo huu unaoendeshwa na Kitengo cha Ulinzi cha Serikali ya Marekani ulianza kutimiwa katika simu mwaka 1990.Teknolojia hii inafanyakazi masaa 24 kwa siku na inauhakika wa kutoa muda halisi wa umbali Fulani,umbali wa mahali kwenda mahali pengine pamoja na kutoa muda wa sehemu mbalimbali za dunia kwa wakati mmoja.

Teknolojia hii iliyopo katika simu za mikononi  inaweza kutumika kuonyesha kifaa kilipo,kitakapokwenda ama kilipo.

Baadhi ya serikali duniani zimetengeneza mifumo yake ya GPS,japo haziingiliani na ule wa awali kwa kweli vinasaidia sana katika kufahamu mahali ulipo.Warusi wanao unaitwa GLONASS na wachina wanayo ambayo mwaka 2012 ilikuwa katika majaribio,Ulaya wanayo inaitwa Galileo na Japani inaitwa Quasi-Zeneth.

Mwaka 2012 Watalaamu wa kuunda wa simu za mkononi walikuwa katika mkakati wa kutengeneza prosessor  ya simu ambayo itakuwa na uwezo wa kutumika katika aina zote za mifumo hii ya kufahama mahali ulipo.

2. Cell ID
 Pamoja na kuwepo kwa teknoloia ya GPS,Makampuni ya kutoa huduma za simu kwa maana ya mitandao ya simu yanafahamu eneo na mahali simu ilipo bila hata ya  GPS,na walifahamu hili hata kabla simu hazijawekewa technolojia hii
Makampuni yanafahamu ni simu ya aina gani mteja anaitumia na umbali gani uliopo kati ya simu na simu nyingine kutokana na teknolojia iitwayo Cell ID ama kitambulisho cha simu,ambapo miongoni mwa vitu vinavyosaidia kufanyakazi kwa teknolojia hii ni minara ya simu. 

3.WI-FI
Wi-Fi inaweza kufanya vyema kwa namna teknolojia ya  Cell ID inavyofanyakazi ,japo si kwa uwezo mkubwa sana kwa kuwa teknolojia ya Wi-Fi inauwezo wa kufanyakazi katika eneo dogo ambapo ni sawa na mita 100.

Teknolojia hii hutumia njia mbili ya kwanza ni ile inayowezesha kuonesha kidokezo cha  uwezo wa kupokea masafa ya mawasilino (RSSI) kwa kutumia masafa ya simu husika kwenye mtandao wa Wi-Fi
Njia ya pili inayotumika katika Wi-Fi ni utumiaji wa alama za vidole ambapo inaelezwa ni njema kwa mtumiaji wa ambaye anapenda kutembelea  eneo fulani mara kwa mara
Alama hizo za vidole zinaweza kutambua mahali ulipo kwa umbali wa mita chache.

4. Bluetooth
Naam utambuzi wa mahali unaweza kufahamika kwenye eneo husika  katika maduka yanayotumia kifaa cha kufahamu na kutunza kumbumbu bei za bidhaa kiitwacho beacons ambacho hutumia teknolojia ya Bluetooth,vifaa hivyo vinaweza kuwasiliana na simu ya mkononi yenye teknolojia ya Bluetooth 4.0.

Hizi ni baadhi tu ya teknojia zilizopo katika simu za kisasa ambazo zaweza kutumika kufahamu simu ilipo na hii inamaanisha kuwa simu ikifahamika ilipo basi hata mtumiaji wa simu hiyo naye anajulikana alipo kumbuka  kadri teknolojia inavyotuweka karibu unaweza kukimbia lakini huwezi kujificha

OBAMA ATADHIBITI UDUKUZI?



Rais Barrack Obama aalitarajiwa juma lilopita kutangaza ambavyo angeweza kurudisha imani katika idara ya ujasusi nchini Marekani kufuatia kufichuliwa kwa taarifa za idara hiyo na aliyekuwa mchambuzi wa maswala ya kijasusi nchini humo Edward Snowden.

Ufichuzi wa hivi karibuni uliochapishwa siku ya alhamisi unadai kuwa idara hiyo ya ujasusi ilidukua mamilioni ya ujumbe katika simu za watu za mkononi duniani kila siku.

Upelelezi huo wa simu zilizopigwa pamoja na mitandao umezua hisia kali kutoka kwa wanaharakati na makundi ya kijamii nchini marekani na washirika wake.

Hata hivyo vitengo vya ujasusi vimeonya kuwa uchunguzi zaidi wa mienendo yake huenda ukaathiri usalama wa marekani.
Chanzo:bbc

Popular Posts

Labels