Thursday, July 17, 2014

ARUSHA:MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UDUKUZI YAPANGWA NA CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA



Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha jijini Arusha kimeanza utaratibu kuwashirikisha watafiti na wabunifu kutoka makundi mbalimbali katika jamii ilikukabiliana na tatizo la Udukuzi wa taarifa za watu kwa vifaa vya mawasiliano vinavyotumia teknolojia mpya ya habari na mawasiliano.

Mkrugenzi wa chuo hicho Bwana Balton Mwamila amesema kuwa ilikufanikisha maadhimio hayo wameamuakuandaa maonesho ya ubuni fu na ugunduziwa teknolojia inayohusu masuala ya kisayansi.

Amesema kuwa bado yapo matatizo yanayo ikabili jamii hasa pale kunako tokea mabadiliko ya kisayansi huku kukiwa hakuna sheria zinazotoa miongozo inayombana mtumiaji wateknolojia mpya hali inayosababisha mtu kuangalia au kudukua taarifazawatu.

Ameeleza kuwakupitia mtandao watu hufahamu undani wa mtu hasa kupitia taarifa zilizohifadhiwa hali aliyoeleza kuwa si sahihi nani hatari kiusalama hasa kwa mwenye taarifa za mtu binafsi.

Aidha swala udukuaji wa taarifa au mawasiliano ya mtu bila ridhaa yamekuwa yakilalamikiwa katika nchi mbalimbali ambapo hivi karibuni nchi ya Uingereza na Ujerumani ziliilalamikia nchi ya Marekani kupitia kikosi chake cha kijasusi kwa kile walichodai kuwa wamedukuliwa taarifa mbalimbali za kimtandao huku nchi nyingi hasa zinazoendelea zikiwa hazina sheria za kuwabana baadhi ya watu wanaotekeleza vitendohivyo.

Saturday, July 5, 2014

MJERUMANI MBARONI KWA KUIFANYIA UJASUSI MAREKANI

Vyombo vya habari vinapasha kuwa, Maafisa nchini Ujerumani wanawashikilia Wajerumani wawili wanaoshukiwa kuifanyia ujasusi na kufanikisha kupenyeza taarifa za siri kwa maafisa wa Marekani, kwa hiyari yao wenyewe.
Steffen Seibert, Msemaji wa Chancellor Angela Merkel, amekiri kutaarifiwa kuhusu suala hilo lililotokea Jumatano ya wiki hii na kusema kuwa Chancellor Merkel alizungumza na Rais wa Marekani, Barack Obama siku ya Alhamisi (ijapokuwa
hakusema ni kipi kilikuwa kiini cha mazungumzo hayo).
Uhusiano baina ya mataifa haya mawili makubwa kiuchumi Duniani umetikiswa kutokana na kuvuja kwa siri za shirika (NSA) lililokuwa likidukua taarifa za mawasiliano nyeti duniani ikiwepo ya Wajerumani na kiongozi wao, Merkel.

Inasadikiwa kuwa mmoja wa waliotiwa mbaroni ni kijana wa umri wa miaka 31, mwajiriwa wa idara ya kiitelijensia ya mambo ya nje ya Ujerumani, aliyenyakua nyaraka za siri 218, ambazo aliziuza kwa $34,000 na kutuma taarifa za Bunge la Ujerumani (Bundestag) kuhusu udadisi wa aina ya maswali yanayokusudiwa kuulizwa ili kupata majibu kuhusu udukuzi wa NSA/Marekani kwa Ujerumani.

Awali, mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa kuhisiwa kuwa anafanyia ujasusi nchi ya Urusi lakini baadaye alikaririwa na chombo kimoja cha habari cha nchini Ujerumani kuwa alikiri kufanyia Marekani ujasusi.

Mtuhumiwa alifikishwa katika korti kuu huko Ujerumani na kuamuriwa kushikiliwa kwa dharura kwa kuwa na nyaraka za kiitelijensia bila ruhusa maalumu. 

Chanzo:http://www.wavuti.com

CRDB YAWATAKA WATEJA WAKE KUWA MAKINI NA MITANDAO YA UHALIFU

Benki ya CRDB imewaonya wateja wake kuwa makini na baadhi ya mitandao inayoibuka na kulaghai kwa kuwataka wananchi,kutoa taarifa zao muhimu za kibenki,jambo ambalo linahatarisha usalama wa fedha zao zinazohifadhiwa na benki hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB,Dr Charles Kimei amesema jijini Dar es salaam hivi karibuni kuwa kumeibuka mchezo kwa baadhi ya mitandao ya kijamii,ikijaribu kuwalaghai wateja kwa kuwaomba taarifa za akaunti zao ili kufanya uhalifu.

Amesema wananchi wanatakiwa kuwa makini na kundi hilo,wasikubali kudanganyika kwa kutoa taarifa zinazohusiana na nyaraka nyeti za benki zao na kusisitiza kuwa ni marufuku kutoa taarifa hizo kwa wafanyakazi wa benki.

Mkurugenzi huyo amesema pamoja na kwamba benki hiyo inawapigia simu wateja wao wakitaka kukamilisha usaili wao kuhusiana na kuingia katika mfumo wa uboreshaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi unaoitwa Simbaking  watambue kuwa hawataulizwa kutoa taarifa zozote za akaunti.

Kuhusu mbinu zinazotumiwa na wahalifu,Mkurugenzi wa Idara Hatarishi James Mabula amesema huwapigia simu wakijifanya kuwa wakurugenzi ama wafanyakazi wa benki hiyo na kisha kuwaghilibu kwa kutaka kupatiwa namba za siri za akaunti husika.



TTCL KUZINDUA KITUO KIKUBWA CHA KUUZIA INTANETI

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) inatarajia kuzindua kituo kikubwa cha kuuzia intaneti Afrika Mashariki mwishoni mwa mwezi julai au Agosti mwaka huu.

Kituo hicho kinatarajiwa kuuza intanet mpaka nje ya nchi,ikiwa ni pamoja na nchi za Malawi,Rwanda,Burundi,Uganda pamoja na nchi nyingine jirani.

Hayo yameelezwa na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni hiyo,Peter Ngota,baada ya kupokea tuzo ya kampuni bora ya mawasiliano.

Amesema kuwa kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa huduma za intaneti ambazo zinawezesha upatikanaji wa huduma za matibabu mtando ambayo yanafanyika katika hospitali mbalimbali nchini.
 

Thursday, July 3, 2014

JKT WAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KUPITIA SMS NA MITANDAO YA KIJAMII



Jeshi la Kujenga Taifa JKT limekanusha taarifa zinazosambazwa kwa njia ya  ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononina mitandao ya jamii kwa  madai ya kuwa vijana wanaofanya mafunzo ya katika makambi ya JKT wanapoteza maisha.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Kanali Erick Komba amesema taarifa hizo si za kweli na zina lengo la kupotosha vijana na watanzania kwa ujumla.

Luteni Kanali komba amesema kifo kilichotokea cha kijana HonorathaValletine Oiso aliyefariki katika kikosi cha JKT Oljoro  mkoani Arusha kilitokana na upungufu wa damu na ugonjwa wa malaria,na si kwa mafunzo ya kijeshi kama ilivyosambazwa kwa njia ya upotoshaji kupitia mitandao.


Wednesday, July 2, 2014

NAULI ZA MATATU NCHINI KENYA KIDIJITALI

Popular Posts

Labels