Vyombo vya habari vinapasha kuwa, Maafisa nchini Ujerumani
wanawashikilia Wajerumani wawili wanaoshukiwa kuifanyia ujasusi na
kufanikisha kupenyeza taarifa za siri kwa maafisa wa Marekani, kwa
hiyari yao wenyewe.
Steffen Seibert, Msemaji wa Chancellor Angela Merkel, amekiri
kutaarifiwa kuhusu suala hilo lililotokea Jumatano ya wiki hii na kusema
kuwa Chancellor Merkel alizungumza na Rais wa Marekani, Barack Obama
siku ya Alhamisi (ijapokuwa
hakusema ni kipi kilikuwa kiini cha mazungumzo hayo).
Uhusiano baina ya mataifa haya mawili makubwa kiuchumi Duniani
umetikiswa kutokana na kuvuja kwa siri za shirika (NSA) lililokuwa
likidukua taarifa za mawasiliano nyeti duniani ikiwepo ya Wajerumani na
kiongozi wao, Merkel.
Inasadikiwa kuwa mmoja wa waliotiwa mbaroni ni kijana wa umri wa miaka
31, mwajiriwa wa idara ya kiitelijensia ya mambo ya nje ya Ujerumani,
aliyenyakua nyaraka za siri 218, ambazo aliziuza kwa $34,000 na kutuma
taarifa za Bunge la Ujerumani (Bundestag) kuhusu udadisi wa aina ya
maswali yanayokusudiwa kuulizwa ili kupata majibu kuhusu udukuzi wa
NSA/Marekani kwa Ujerumani.
Awali, mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa kuhisiwa kuwa anafanyia ujasusi
nchi ya Urusi lakini baadaye alikaririwa na chombo kimoja cha habari cha
nchini Ujerumani kuwa alikiri kufanyia Marekani ujasusi.
Mtuhumiwa alifikishwa katika korti kuu huko Ujerumani na kuamuriwa
kushikiliwa kwa dharura kwa kuwa na nyaraka za kiitelijensia bila ruhusa
maalumu.
Chanzo:http://www.wavuti.com
Popular Posts
-
anzania imejaaliwa kuwa na kampuni na taasisi kadhaa zinazohusika na mawasiliano na nyingi ni binafsi zinazojiendesha kwa faida kubwa kabisa...
-
SERIKALI YA TANZANIA YASEMA:KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAITAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Jana na leo, Serikali ya Tanzania imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunza...
-
Afisa wa Taasisi ya uwezeshaji na ujengaji uwezo kwa wateknohama nchini KINU, Catherinerose Barretto akimkabidhi cheti Ally Said toka P...
-
Wapiga kura 2,845,256 wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa mwili wa binada...
-
Serikali ya Tanzania inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hivi karibuni kumezuka kundi la Watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakit...
-
Kanisa la River Side lililopo mtaa wa Njiro jijini Arusha, Tanzania, limetangazwa kuwa ni kanisa pekee barani Afrika ambalo limefikia...
-
Lagos, Nigeria - A little over a decade ago there were about 100,000 phone lines in Nigeria, mostly landlines run by the state-owned tel...
-
Watafiti toka kampuni ya utafiti ya Zscalar wamegundua kuwa,tovuti za kichina zenye picha za ngono zimekuwa zikisamb...