Wednesday, February 11, 2015

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO RIVER SIDE ARUSHA LASHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KUTUNZA KUMBUMBUMBU ZA WASHIRIKI KITEKNOHAMA


 

Kanisa la River Side lililopo mtaa wa Njiro jijini Arusha, Tanzania, limetangazwa kuwa ni kanisa pekee barani Afrika ambalo limefikia asilimia 80 ya kutunza kumbukumbu za majina ya washiriki kwa kutumia mfumo wa kiteknolojia ya habari na mawasiliano  wa usimamizi wa makanisa ya kiadventista.



Taarifa hiyo imetolewa  na Msimamizi mkuu wa mfumo wa Usimamizi wa makanisa ya kiadventista duniani Mrs Sherri Ingram-Hudgins Februari 9, mwaka huu wakati akitoa takwimu za mfumo mpya wa kanisa la Waadventista wa kusimamia makanisa (ACMS) kwenye mkutano wa wanateknohama wa kanisa hilo uliofanyika Maryland,Silver Spring,Marekani.

                                                                                                                                           

Takwimu hizo zinaonesha kuwa  Brazil ndio inaongoza duniani kuwa na washiriki wengi waliosajiliwa, ikifuatiwa na nchi za Peru na Argentina. Barani Afrika, Tanzania ndio inaongoza ikifuatiwa na Ghana.

Mwaka 2015, mfumo huu unategemewa kuanzishwa katika nchi za Kenya, Africa Kusini na Madagascar.


Akieleza mbele ya wajumbe kutoka division 13 duniani, Sherri alionesha jinsi mfumo huu wa kusimamia makanisa ulivyoboreshwa kwenye vipengele 5 ambapo unauwezo wa kutunza kumbukumbu za vikao vya kanisa mahalia, kupiga kura za kuchagua viongozi wa kanisa, unawezesha kanisa mahalia kuufasiri kwa lugha husika ya kanisa mahalia ,kutunza kumbukumbu za fedha za kanisa na kukusanya taarifa za kila idara kisha kuzituma konferensi, unioni, divisheni na Konferensi Kuu.



Awali mfumo huu ulipoanza kutumika ulikuwa na uwezo wa kutunza majina ya washiriki na kuhamisha jina la mshiriki toka kanisa moja kwenda jingine.



 Sherri ametoa rai kwa wajumbe wote kuusimamia mfumo huu kwa makanisa yote makubwa yaliyopo mijini kisha kwenda makanisa yaliyopo vijijini.



Divisheni ya  Afrika mashariki na kati iliwakilishwa na wajumbe watatu, Nicolas Washington (Kenya), Kelvin Opiyo (Kenya) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Unioni Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania  Gideon Msambwa.








Popular Posts

Labels