Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema hajapokea maombi ya Chama
cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania nchini Tanzania (MOAT) kuhusu kusitisha
kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokana na kushindwa
kumudu gharama za uendeshaji wanazodai zinatokana na urushaji wa matangazo kwa njia ya dijitali.
Kupitia kipindi cha Radio One asubuhi ya leo,Waziri Mbarawa amesema hajapokea ombi hilo ambalo hafahamu linaeleza nini na atakapolipokea wizara italifanyia kazi japo amesema wamiliki wa vituo vya televisheni nchini walikubaliana na wizara katika uhamishaji wa masafa ya utangazaji kutoka analojia kwenda dijitali mchakato ambao ulianza mwaka 2005 na vyombo hivyo vilikubali kutumia teknolojia hiyo.
Kabla ya kuanza kwa zoezi la kuzima mitambo ya analojia disemba 31,2012 vyombo vyote vya utangazaji viliitwa na kusaini makubaliano ya kuzima mitambo na kuanza kurusha kwa njia ya dijitali.
Nayo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema haitarudi nyuma kwenye suala
la kutumia mfumo wa matangazo kupitia njia ya dijitali na kwamba mfumo huo
utaendelea kutumika.
TCRA ilizima mitambo ya analojia na kuhamia dijitali, Desemba 31, mwaka jana
kitendo ambacho Chama
cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) wanadai kimepunguza mapato yanayotokana na matangazo.
Popular Posts
-
SERIKALI YA TANZANIA YASEMA:KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAITAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Jana na leo, Serikali ya Tanzania imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunza...
-
Facebook wametangaza kitu kipya kwa simu za Android walichokipa jina la Home. Kwa muda mrefu kulikuwa na uvumi kuwa Facebook wana...
-
Microsoft is switching off its Windows Live Messenger service on 15 March. On that date Messenger log-ins will no longer work a...
-
Watu wengi wameshaona filamu ambazo wahalifu wakidukua simu za mikononi hata kama zimezimwa. Kama ili...
-
Na Yusuph Kileo Nchi ya Tanzania yabahatika tena kwa mara ya tatu kuwa mwenyeji wa mkutano wa “Connect 2 Connect” ambapo kauli mbiu ya...
-
Kanisa la River Side lililopo mtaa wa Njiro jijini Arusha, Tanzania, limetangazwa kuwa ni kanisa pekee barani Afrika ambalo limefikia...
-
Lagos, Nigeria - A little over a decade ago there were about 100,000 phone lines in Nigeria, mostly landlines run by the state-owned tel...