Tuesday, April 29, 2014

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA VIVINJARI VYA “INTERNET EXPLORER”

 

Mwishoni mwa juma lililopita pamegundulika hali mbaya ya kiusalama mtandao itakayo waathiri watumiaji wa kivinjari kijulikanacho kama "internet explorer" ambapo watumiaji wa kivinjari hicho wako hatarini kuweza kuingiliwa kirahisi computer zao na wahalifu mtandao.

Jumamosi iliyopita tangazo hilo linalosomeka hapa "TANGAZO" limeweza kubainisha internet explorer toleo la sita (6)  hadi la kumi na moja (11) yote yameweza kugundulika yanatoa mwanya kwa wahalifu mtandao kupenya kwa watumiaji na kuchukua taarifa zozote zitakazo patikana kwenye computer zao.



Aidha, Kampuni inayojihusisha na na maswala ya ulinzi mtandao ya "FireEye" imeonyesha takwimu yakua asilimia 56 ya vivinjari, hadi ilipofikia mwaka 2013 vilikua hatarini kuingiliwa na wahalifu. Na kubainisha kwamba wahalifu wamekua na uwezo wa kutengeneza vivinjari visivyo sahihi vinavyo weza ruhusu wahalifu hao kuingilia computer za watu mara tu watumiaji wa vi vinjari hivyo wanapo vitumia.



Microsofti imeshindwa kupata suluhu ya tatizo hilo ambapo CERT ya marekani imetoa tahadhari inalosomeka hapa "CERT ALERT" yakuwa watumiaji vivinjari vya "internet explorer" wanapaswa kubadili vivinjari kwa sasa na badala yake watumie vingine kama vile (Mozilla fox, Google chrome n.k) hadi hapo tatizo litakapo rekebishwa na kutangazwa vingenevyo.



Aidha,Christian Tripputi Ametumia muda huu kuonya watumiaji wa Window XP yakuwa kwa sasa wako hatarini kwani hakuna tena huduma zitakazo endelea kutolewa kwa Window hiyo na wahalifu mtandao wamesha anza kuleta madhara kwa wote wanaoendelea na matumizi ya windo hiyo na kusisistiza hapata kuwa na msaada kwa waathirika.

Taarifa ya kingereza inasomeka inapatikana hapa




 

Monday, April 28, 2014

SHULE YA TASS YAPATA KOMPUTA 50

Shule ya sekondari ya Waadventista Wa Sabato  {Tass} imepokea jumla ya komputa hamsini zitakazotumika katika mafunzo ya utafiti kivitendo katika maabara ya kisasa ya sayansi iliyozinduliwa hivi karibuni.
 

Hayo yamesemwa na mkuu wa shule hiyo mwl joseph kehengu wakati akiwasilisha taarifa ya shule kwa mgeniRasmi,wanahabari,wanafunzi na wazazi kwenye mahafali ya kwanza ya kidato cha sita Tangu shule ianzishwe mwka 1999.Bwana joseph alisema kuwa computa hizo zilizotolewa na mmiliki wa shule hiyo ambaye ni kanisa la waadventista wasabato Tanzania zitaleta mwamko mkubwa na hamasa kwa wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na zitawezesha utafiti wa maswala ya kisayansi kufanyika kwa ufanisi zaidi.
 

Kwa upande mwingine akijibu risala ya wanafunzi pamoja na taarifa ya mwalimu mkuu wa shule katika mahafali ya kwanza ya kidato cha sita yaliyofanyika jana April 27 /2014 Mgeni rasmi katika mahafali hayo ndugu Wilson Kabwe mkurugenzi wa jiji la 
Dar es salaam awaasa wanafunzi wahitimu kutoridhika na kiwango walichofika badala yake awasonge mbele zaidi kielimu.

           

WASHIRIKI WATAKIWA KUTOA SADAKA NA MICHANGO KWA KUTUMIA SIMU NA TAASISI ZA KIBENKI



Uongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai umewataka washiriki wa kanisa hilo kutumia taasis za kibenki na mifumo ya kuhamisha pesa kwa njia ya mitandao ya simu katika utoaji wa sadaka na michango ya kanisa ili kuepukana na uhalifu wa fedha.

Usiku wa kuamkia April 24,mwaka huu kati ya saa 9 hadi saa 10 alifajiri watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia Kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai na kupora kasha la fedha,projekta moja ,nyalaka muhimu za kanisa na kufanya uharibifu wa ofisi ya mchungani wa kanisa hilo.

Akitoa taarifa ya uongozi wa kanisa kwa washiriki siku ya sabato,Mzee Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai,Msafiri Mbibo amesema imefikia wakati sasa kwa washiriki kutumia mifumo ya kisasa ya mitandao ya simu katika utoaji wa sadaka ama michango ambayo itakuwa ikiwekwa kwenye taasisi za kibenki moja kwa moja ili kuepusha uhalifu kanisani hapo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa kanisa hilo lina mfumo wa utunzaji wa taarifa za kifedha wa teknolojia ya habari na mawasiliano ambao haukuathiriwa na uharibifu uliotokea kanisani hapo.

Kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai lilijengwa mwaka 1963,na sasa liko katika mchakato wa ujenzi wa kanisa kubwa  linalokadiriwa kugharimu takribani shilingi bilioni 3 za kitanzania.




Friday, April 25, 2014

MITAMBO YA ANALOJIA KUZIMWA BUKOBA NA MUSOMA APRIL 30 MWAKA HUU

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kuzima rasmi mitambo ya analojia ya urushaji wa matangazo ya televisheni katika miji ya Bukoba mkoani Kagera na Musoma,Mara mwishoni  mwa mwezi huu.
Naibu Mkurugenzi Idara ya Utangazaji wa Mamlaka hiyo,Frederick Ntobi amesema zoezi hilo la uzimaji wa mitambo hiyo na kuhamia dijitali katika miji hiyo litaendeshwa saa 6:00 usiku.
Kwa mujibu wa Ntobi,zoezi hilo litahusisha mitambo inayotumia mfumo wa satelaiti,matangazo kwa njia ya waya au mitambo ya radio. Amesema uzimaji wa mitambo hiyo ni awamu ya pili baada ya kwanza kuhusisha mikoa ya Dar es salaam,Mbeya,Tanga,Mwanza,Arusha na Mbeya.
Aliwataka wakazi wa wilaya hizo za Bukoba na Musoma kuhakikisha wananunua ving'amuzi ili waweze kuangalia vipindi mbalimbali vya kwenye televisheni.

BANDARI ZA TANZANIA KUANZA MAJARIBIO YA MFUMO WA KITEKNOHAMA IFIKAPO JUNI 2014

Tanzania iko katika hatua muhimu ya utekelezaji wa mfumo wa kompyuta katika utoaji wa mizigo(National Electronic Single Window System) katika bandari, majabio ya mfumo huu yataanza mwezi Juni 2014, ili kurahisisha ufanyaji biashara na kuchangia kuinua uchumi wa Tanzania.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Bandari Phares Magesa amesema Mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa niaba ya wadau wote na utanufaisha watumiaji wa bandari zote, viwanja vya ndege, mipaka yote ya Tanzania. Mfumo huu unatarajiwa kupunguza muda wa mizigo kukaa bandarini na hivyo bidhaa kuingia katika mzunguko wa uchumi haraka. 



Wadau wa Port Community System wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao mapema juma hili.


Mwenyekiti wa wadau Ndg. Igogo kulia akijadiliana jambo na Ndg. Magesa  kwa niaba ya wadau wote wa Bandari, kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Phaeros Group ya Ubelgiji ambao ndio watengenezaji wa mfumo huo. 

MTANDAO WA TIGO KUTOA HUDUMA YA FACEBOOK KWA LUGHA YA KISWAHILI


Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez (Kushoto) akipongezana na  Mkurugenzi wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa wa Facebook Nicola D'Eli baada ya kuzindua huduma ya Facebook bila malipo kwa lugha ya kiswahili kupitia mtandao wa Tigo (Picha na Tigo Tanzania)

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania imezindua mpango wa kutoa bure huduma za mtandao wa kijamii wa Facebook kwa lugha ya kiswahili .

Huduma hiyo inatolewa kwa mara ya kwanza,itawanufaisha wateja wake waote nchini Tanzania na wale wa nchi zingine za Afrika Mashariki.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Dar es salaam jana,Mkurugenzi Mkuu wa Tigo,Diego Gutierrez alisema ushirikiano huo utawawezesha wateja wanaotumia mtandao wa Tigo kuperuzi kwenye facebook kupitia simu zao za mkononi bila gharama zozote na kwa lugha ya kiswahili badala ya kiingereza.

Tanzania itakuwa ni nchi ya Pili kupata nafasi ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo,Paraguay ilikuwa ya kwanza kupata huduma sawia na hiyo ambayo ilizinduliwa Desemba mwaka jana na watumiaji wa mtandao huo wanatumia lugha ya Kiguarani.

Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watu wanaotumia mtandao wa Facebook nchini Tanzania ni milioni 2 ,huku kukiwa na idadi ya watumiaji wa mtandao huo bilioni 1.2 duniani.

Thursday, April 24, 2014

CHINA YAZIFUNGIA TOVUTI 110 ZINAZOONESHA MASUALA YA NGONO


China imezifungia tovuti 110 ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kuzuia masuala ya ngono kwenye mitandao.Imeeleza taarifa ya serikali hiyo inayosimamia masuala ya taarifa mitandao iliyotolewa juma hili.

Mitandao ya kijamii 3,300 inayotoa huduma nchini China ,ikiwemo WeChat na Sina Weibo na majukwaa ya kijamii kwenye mitandao yameondolewa katika kampeni iitwayo
"Cleaning the Web 2014".

 
Karibu matangazo  7,000 na ujumbe wa maneno 200,000 wenye aina za maneno ya ngono vimeondolewa.

Kampeni hiyo ni sehemu ya utaratibu wa kuondoa usambaaji wa mitandao ya ngono katika nchi hiyo ambayo hadi kufikia mwezi disemba 2013 ilikuwa na watumiaji wa intaneti wapatao milioni 618,ambapo mwaka 2012 ilizifungia blog 97,000 kutokana na kujihusisha na uandikaji wa habari za ngono.

Chanzo:Xinhua

Friday, April 18, 2014

SERIKALI YA TANZANIA KUANDAA SHERIA YA KUKABILIANA NA UHALIFU WA KIMTANDAO

Serikali ya Tanzania ipo katika hatua ya mwisho za kuandaa sheria ya kukabiliana na uhalifu wa kimtandao ambapo kwa sasa inajiandaa kuwasilisha muswaada wa sheria hiyo kwenye baraza la Mawaziri.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Tanzania Profesa Makame Mbarawa wakati akizungumza kwenye baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo.


Profesa Mbarawa amesema kuwa sheria tatu zinatarajia kutengenezwa kupitia mpango huo wa kukabiliana na uhalifu wa mitandao zitagusa maeneo muhimu yatakayotumia mitandao hususani huduma za fedha kwa mtandao


Ameitaja mikakati mingine inayofanywa na serikali katika kuboresha sekta ya mawasiliano na teknolojia kuwa ni pamoja na uwekezaji utaogharimu kiasi cha fedha shilingi ishirini na uendelezaji wa ujenzi wa mkongo wa taifa wa mawasiliano.


Aidha amewataka watumishi wa Wizara hiyo kujadili namna ya kuboresha utendaji kwenye wizara bila ya kuwa na vitengo vingi akiwataka kuunganisha idara zitakazoshabihiana katika utendaji bila kutanguliza maslahi binafsi.

Wednesday, April 16, 2014

SERIKALI YA TANZANIA YAINGIA MKATABA WA MRADI WA MTANDO WA MAWASILIANO KATIKA TAASISI ZAKE

Serikali,Kampuni ya Simu nchini Tanzania TTCL na kampuni binafsi ya mawasiliano ya Soft Net,imetiliana saini mkataba kuendesha miradi ya utekelezaji wa mtandao wa mawasiliano serikalini.

Naye Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi amesema mtandao wa mawasiliano wa serikali ni muhimu kwani utasaidia kupanua wigo wa mawasiliano na pia kuwa kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania.

Mradi huo una lengo la kuunganisha taasisi za serikali pamoja na kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi za kwa haraka.
Kwa upande wao wawakilishi wa TCCL na Soft Net wamesema mradi huo unatajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 za kitanzania utahudumia taasisi 72 za Wizara,idara 19 zitakazojitegemea pamoja na wakala 30 za serikali.

Thursday, April 10, 2014

UMAKINI KATIKA KUTOA TAARIFA BINAFSI MITANDAONI




Displaying 1.jpg
 
 Displaying 2.jpg

 Displaying 3.jpg

Katika Muendelezo wa Kuelimisha Jamii jinsi ya kubaki salama mitandaoni leo najikita katika maswala ya USIRI “PRIVACY” ambapo taarifa nyingi za mtu binafsi si vyema kuwekwa mitandaoni napia maelezo mafupi ya namna wahalifu mtandao wanatumia taarifa hizo za siri mitandaoni kuleta madhara.

Njia za awali ambazo wahalifu mtandao wanatumia kabla ya kusababisha madhara ni kukusanya taarifa za mhusika ambaye wanategemea kumdhuru kwa njia inayojulikana kitaalam kama “RECONNAISSANCE” ambapo mara nyingi taarifa za awali zinapatikana kwenye mitandao ya kijamii kwani inaaminika wengi hawana umakini katika kutoa taarifa zao kupitia mitandao ya kijamii.

Jamii inashauriwa kujenga umakini wa taarifa binafsi wanazo ziweka mitandaoni ili kuweza kubaki salama. “Takwimu inaonyesha asilimia kubwa ya watumiaji wamekuwa wakiweka taarifa ambazo zinaweza kutoa urahisi wakugundua mambo mengi kutoka kwa muhusika” – Yusuph Kileo.

Mfano, Kuna wale ambao hadi leo wanatumia maneno ya siri “PASSWORDS” kwa kutumia mwaka wao wa kuzaliwwa wakati kuo huo mwaka huo wa kuzaliwa umewekwa kwenye mitandao ya kijamii hapo inaonyesha ni jinsi gani muhusika huyu anatengeneza urahisi kwa mhalifu kuweza kumuingilia kumdhuru.

Aidha, Umuhimu mkubwa unahitajika katika utoaji wa siri za mtu binafsi kwani panapokua na ugumu katika kukusanya taarifa za awali za mtu binafsi kunajengeka ugumu wa ukusanyaji wa taarifa za muhusika ambapo kunapelekea ugumu kwa mhalifu kuleta madhara kirahisi kwa mhusika.
Pia Kumekua na wimbi la wahalifu wanao omba moja kwa moja kupitia baruapepe au mitandao ya kijamii taarifa za watu na takwimu zinaonyesha kuna wale ambao bado wanatoa taarifa hizo bila kujua athari zake.

“Nashauri Unapo pokea jumbe inayo kuhitaji utoe taarifa zako binafsi aidha kwa maelezo kuwa kuna matengenezo katika akaunti yako au kukuwezesha kifedha na kuanzisha uhusiano kuwa makini kwani ni moja ya hatua za ukusanyaji wa taarifa za mtu ili kujenga njia ya kuanzisha madhara” – Yusuph Kileo.


TAHADHARI NA MTANDAO WA UTAPELI UNAOJIITA TCRA FOUNDATION

Mamlaka ya Mawasiliano imebaini kuwa kuna mtandao wa matapeli wanaotumia jina la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutumia tovuti inayojiita “TCRA Foundation” na inayodanganya kutoa mikopo kwa maendeleo kwa watu.

Mtandao huu umetengenezwa wa kutumia picha zilizopo kwenye mitandao mbalimbali zikiwaonyesha Raisi Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Makawe Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Prof. John Nkoma.

Aidha mtandao huu unadai kuwa Mamlaka kwa kushirikiana na Kampuni za Simu za Vodacom na Tigo pamoja na Benki ya CRDB na NMB zinashirikiana kuendesha Foundation hiyo.

Mamlaka ya Mawasiliano inawatahadharisha wananchi kuwa haina “Foundation” yoyote ya kutoa misaada ya fedha. Mtandao huu unatumika kuwalaghai wananchi na kuwaibia fedha zao kwa kuwataka watume fedha za kujiunga na mtandaqo huo kwa number za simu za Tigo na Vodacom zinazoonesha kusajiliwa kwa jina la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Sio kweli na ni wizi na udanganyifu.

Mamlaka ya Mawasiliano inawataka wananchi kuwa na tahadhari na watu hawa ambao hutumia mitandao ya Mawasiliano ya simu na intaneti kufanya utapeli. Usitume fedha wala kujiunga na mitandao ya namna hii.

Aidha Mamlaka ya Mawasiliano inawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa wanapobaini utapeli wa namna hii kwa kutoa taarifa kwa Mamlaka kwa vyombo vingine vya usalama ikiwa watahisi au kuwa na taarifa za watu wanaojihusisha na udanganyifu huu katika mitandao ya Mawasiliano ili kuzuia vitendo hivi vilivyoshamiri katika siku za hivi karibuni.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Saturday, April 5, 2014

TAHADHARI DHIDI YA UHALIFU UNAOFANYWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kuzingatia kifungu 5 (b) na (e) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya 2003 inatoa tahadhari kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano, wananchi na umma kwa ujumla kujihadhari na utapeli unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi na mtandao wa intaneti kama ifuatavyo:

1. Usimpe mtu yeyote usiyemfahamu vizuri simu yako au kadi yako ya simu ili atumie.

2. Usitoe maelezo yoyote kuhusu namba yako ya simu au taarifa za binafsi kwa mtu yeyote anayekupigia simu kutaka taarifa hizo.

3. Usijibu ujumbe wa simu unaohusiana na fedha zako hata kama namba iliyotuma unaifahamu.

4. Usitekeleze maagizo yoyote yanayohusu fedha kwa ujumbe wa maandishi hata kama yanatoka kwenye namba ya mtu unayemfahamu. Mpigie aliyekutumia ujumbe uzungumze naye.

5. Usitekeleze maagizo yoyote kutokana na ujumbe wa simu za mkononi unaokutaka kutuma fedha kutoka namba ambayo mtumiaji wake unamfahamu na ambao unakueleza kwamba simu yake ina hitilafu hivyo hawezi kuongea, usitekeleze maagizo hayo.


6. Ukipata ujumbe kwamba umepokea fedha kwa njia ya simu, mpigie aliyekutumia na usitoe pesa hizo hadi uthibitishe kwamba zimetumwa kwa nia njema.

7. Weka njia za kuthibitisha taarifa kabla ya kufanya miamala ya kifedha kutumia simu ya mkononi.

8. Ukipigiwa simu na mtu yeyote kuhusu masuala ya fedha, hata kama unadhani unamfahamu mtu huyo; mpigie tena kwa namba yake unayoijua ili kuhakikisha kwamba ni yeye.

9. Iwapo unafanya biashara ya huduma za simu hakikisha kwamba simu unayoitumia kwa miamala ya kifedha ni tofauti na unayotumia kwa shughuli nyingine na hakikisha simu hiyo haitumiwi na mtu mwingine

10. Tumia namba ya siri ambayo sio rahisi mtu mwingine kukisia.

11. Usitoe namba zako za siri unazotumia kwa huduma

12. Thibitisha na hakiki namba ya mtu unayemtumia pesa au salio kabla ya kutuma

13. Ukipoteza simu au laini yako ya simu toa taarifa kwa mtoa huduma wako na Polisi mara moja.

14. Ukifanyiwa uhalifu ambapo simu au mtandao umetumika kufanyia uhalifu huo hilo nikosa la jinai. Toa taarifa Polisi ili wahalifu wasakwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

15. Usipopata ushirikiano wa kutosha kwa mtoa huduma wako katika kutatua taizo lako wasilisha malalamiko yako Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Unaweza kuwasilisha malalamiko kwa kutuandikia ( S.L.P 474 Dar Es Salaam); kufika ofisini makao makuu namba 20 Sam Nujoma Dar es Salaam au kwenye ofisi za Kanda na Zanzibar; kupiga simu ( namba 0784 558270 au 0784 558271) na kwa barua pepe ( malalamiko@tcra.go.tz au complaints@tcra.go.tz)


Imetolewa na: MKURUGENZI MKUU, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

KWANINI UNAHITAJI UPDATES ZA KOMPYUTA/SIMU?


Watu wa TEKINOHAMA haswa wanaohusika na masuala ya Ufundi au kusimamia masuala ya usalama huwa wanaulizwa maswali 2 sana .

Hivi naweza kutumia Kompyuta yangu bila kufanya updates ?

Naweza kupata Antivirus ambayo hainiulizi/Haitaki updates ?

UPDATES KATIKA KOMPYUTA/SIMU NI NINI ?

Updates ni zile programu zinazoingizwa au ingia kwenye kompyuta yako au simu yako kwa ajili ya kuboresha programu za kompyuta yako au simu yako .

Kama ulinunua kompyuta ikawa na programu inayoitwa UJAMAA 1.2 , Baada ya mwaka au miezi kukiwa na UJAMAA 1.3 basi hii ndio update ya toleo 1.2 , update hii unaweza kuipata bure au kulipia kulingana na Kampuni yenyewe lakini update nyingi ni bure .
Kuweka updates ni sawa na mwanadamu anavyokula vyakula ili aweze apate afya aweze kuendelea kuishi na kufanya shuguli zake mbalimbali za kujipatia kipato .

UPDATES ZINAPATIKANAJE ?

Kuna njia 2 za kupate updates :-

1 - Kwa Njia ya Mtandao( Moja Kwa moja ) - Hii inatumika kama kifaa chako kimeunganishwa kwenye mtandao na umekiruhusu kupokea updates kwa njia za mtandao , mara nyingi updates hizi kufanya moja kwa moja ikimaliza inaingiza yenyewe kwa kuinstall .
Njia hii inakuunganisha moja kwa moja na mtengenezaji wa programu husika .

2 - Kwa Njia ya Download - Hii ni kwa watu wasiokuwa na huduma ya mtandao lakini wanataka kupata update fulani au wakati mwingine mtu shirika lina kompyuta 200 na zote wanataka kuweka update moja lakini bila kuunganisha kwenye mtandao , unachofanya ni kwenda kwenye tovuti husika ya programu utapata update hiyo na utapata maelezo ya jinsi ya kuitumia .

Hii unaweza kufanya hata kwenye internet cafe yenye kompyuta nyingi au ofisi zenye kompyuta nyingi kwa kudownload file moja ambalo utaweza kutumia kwenye zote .

3 - PATCH - Hizi ni updates pia lakini lengo lake haswa ni kurekebisha kosa ambalo lilifanyika wakati wa utengenezaji wa programu hisika , hii nayo ni bure kwa programu nyingi .

4- Plugins - Hivi ni viongo/Viongezeo katika programu mbalimbali za kompyuta au simu kwa ajili ya kuboresha utendaji wa kitu fulani , hizi zinatumika zaidi kwa watu wa uhandisi na uchoraji au uchanganyaji picha , utakuta kuna kitu anahitaji kufanya kutumia programu yake badala ya kuwa na programu fulani kubwa basi ataweza kupata Plugin moja ndogo ya kufanya kitu hicho specific .

Tafadhali usitumie Plugin kama hujui unachofanya ni rahisi kukuharibia mambo yako

UPDATE HUFANYIKA BAADA YA MUDA GANI ?

Kila kampuni inayotengeneza bidhaa ina sera zake kuhusu updates lakini kila zinapotoka huwa kwenye mtandao wa kampuni husika kama ulikosa unaweza kutafuta ukapata lakini kama umenunua kompyuta leo au simu ukijiunga tu utalazimika kupata updates zote zilizopita mpaka leo vile vile kwa antivirus na Simu .

Mara nyingi
Zaidi unaweza kufuatilia vyombo vya habari na kusoma kwenye mitandao kama kuna updates zozote kuhusu programu husika .

MUHIMU

Kompyuta nyingi zenye programu ambazo sio halali wanaogopa kufanya updates kwa hofu kwamba atakamatwa au itafanya hili na lile , bora upate ujumbe kwamba unatumia programu bandia na uendelee kuitumia kuliko kutokufanya updates kabisa kwa sababu utakuwa unabadilisha mafundi kila siku na itakuwa rahisi kwa kifaa chako kushambuliwa au watu kutumia kama mlango wa kufanya mashambulizi kwenye mitandao mingine .

Kama mko maofisini au majumbani ni vizuri muwe na sheria kali kuhusu kufanya updates za vitu mbalimbali vinavyotumia programu maana itakuwa nafuu na ulinzi tosha kwako na kwa mali zako .

Kuna watu wanaibiwa data zako kwenye kompyuta kwa sababu tu hakufanya updates kwenye antivirus yake matokeo yake alipoingia kwenye kompyuta spyware wakaingia wakaweza kutumiwa kuhamisha taarifa au mambo mengine .
YONA F MARO
0786 806028
 

Tuesday, April 1, 2014

SERIKALI YA TANZANA YAWATAHADHARISHA WANANCHI KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA TEKNOHAMA

Serikali ya Tanzania imewatahadharisha wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKINOHAMA) ili kuondoa vitendo vya uhalifu hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi Prisca Ulomi wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Akifafanua Bi Prisca amesema kuwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa kutambua umuhimu wa TEKINOHAMA wameamua kuandaa muswada wa Sheria za Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao (Cyber Laws).

Akieleza zaidi Bi Prisca amesema kuwa Muswada wa sheria hizo ni pamoja na Muswada wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi (The Personal Data Protection Bill), Muswada wa Sheria ya Biashara ya Miamala ya Kielektroniki (Electronic Transaction Bill), na Muswada wa Sheria ya Kuzuia Uhalifu kwa njia ya Kompyuta na Mtandao (Computer and Cyber Crimes Bills).

“Sheria hizo zitasaidia kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini kwa kudhibiti uhalifu kwa kutumia mitandao na kuwalinda watoto dhidi ya matumizi yasiyofaa ya mitandao”. alisema Bi Prisca.

Bi Prisca aliongeza kuwa serikali imetumia gharama kubwa kuweka miundombinu ya TEHAMA ambayo imesaidia kuboresha na kuharakisha utoaji wa huduma mbalimbali na kubainisha kuwa wapo baadhi ya watu wanatumia vibaya teknolojia hiyo, hivyo kuna umuhimu wa kuwepo sheria zitakazodhibiti uhalifu kupitia mitandao.

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia imetoa rai kwa wananchi kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao na badala yake watumie vizuri mitandao hiyo kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla hali inayoweza kuathiri ukuaji wa sekta hiyo nchini.

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU KUVURUGA PROGRAMU YA WINXP

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU KUVURUGA PROGRAMU YA WINXP

1 – PROGRAMU YA WIN XP KUVURUGIKA 
Sio ukweli kwamba programu ya win xp itavuruguka kama inavyoelezwa na watu wengi .
2 – KITAKACHOTOKEA 
Microsoft itaacha kutoa baadhi ya huduma za kuboresha windows xp kwa jina lingine ni updates ambazo zilikuwa zinapatikana pale mtu anapojiunga kwenye mtandao bure .
Unapokosa hizi updates maana yake windows xp yako inakuwa haikostable kupambana na mengine yanayoweza kutokea kwenye kompyuta yako haswa upande wa software , kwahiyo updates ni sawa na mtu anavyokula chakula kunachoenda kuboresha afya yake aweze kuendelea kuishi na kufanya shuguli nyingine .

3 – VIPI PROGRAMU NYINGINE 
Kampuni nyingi za program zimeboresha na zinaendelea kuboresha program zao ili ziweze kufanya kazi na operating system mpya za zilizoboreshwa zaidi kama windows 7 , 8 , 8.1 ETC .

Mfano sasa hivi kuna printa ambazo hazina program za win xp kwahiyo ukiwa na win xp huwezi kutumia printa hizo .

4- KWA WANAOENDELEA KUTUMIA WINDOWS XP
Kama nilivyoeleza Microsoft haitokuwa inatoa msaada na updates za kuboresha windows xp , ili uhamie windows 7 , 8 na nyingine zilizokuwepo katika matumizi , hii ina maanisha Microsoft haitahusika na suala lolote la kisheria litakalotokea endapo utaendelea kutumia .

5 – WENGINE WAMEFANYAJE ?
Kuna baadhi ya kampuni zimeingia mkataba na Microsoft kwa ajili ya kuendelea kuhudumia windows xp zao huku wao wakiendelea kufanya mchakato wa mabadiliko kidogo kidogo kulingana na uwezo wao wa kifedha na sera za kampuni , sherika au nchi husika , kwa Tanzania watu wangejaribu kuwasiliana na ofisi za Microsoft nchini Kenya hawa wanaweza kuwapa msaada zaidi haswa kwa mabenki na huduma nyingine kubwa kubwa .

6 – TATIZO LA AFRIKA NA NCHI MASIKINI 
Hizi program za windows xp , windows 8 na 7 ni gharama sana , kwa mfano windows 7 kwa Tanzania ni dola 250 hivi ukichanganya na office unapata dola 500 ukiweka na antivirus ni dola 550 hiyo ni kama ukiamua kununua genuine na DVD zake , hii watu wengi hawana uwezo wa kununua na hizi serikali zetu na uwezo wao ni mdogo , kuwapeleka huko juu ni gharama zaidi kwa watu na serikali .

USHAURI WANGU 
Serikali iingie mikataba na kampuni zinazouza program zao kwa wingi nchini Tanzania haswa Microsoft , adobe , apple , kaspersky , Symantec , oracle , ETC ili waweze kufanya mipango ya kupunguza bei kwa ajili ya soko la Tanzania hii itasaidia watu kupata program halisi kwa bei nzuri kidogo na zenye uhakika bila hivyo wananchi watakimbilia kwenye program ambazo sio halisi na wataendelea kutumia gharama kubwa kwenye matengenezo na kukumbana na karaha nyingine za kihalifu .

YONA F MARO 
O786 806028

Popular Posts

Labels