Mamlaka
ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kuzima rasmi mitambo ya
analojia ya urushaji wa matangazo ya televisheni katika miji ya Bukoba mkoani Kagera na Musoma,Mara mwishoni
mwa mwezi huu.
Naibu
Mkurugenzi Idara ya Utangazaji wa Mamlaka hiyo,Frederick Ntobi amesema
zoezi hilo la uzimaji wa mitambo hiyo na kuhamia dijitali katika miji
hiyo litaendeshwa saa 6:00 usiku.
Kwa mujibu wa Ntobi,zoezi hilo litahusisha mitambo inayotumia mfumo wa satelaiti,matangazo kwa njia ya waya au mitambo ya radio.
Amesema
uzimaji wa mitambo hiyo ni awamu ya pili baada ya kwanza kuhusisha
mikoa ya Dar es salaam,Mbeya,Tanga,Mwanza,Arusha na Mbeya.
Aliwataka
wakazi wa wilaya hizo za Bukoba na Musoma kuhakikisha wananunua
ving'amuzi ili waweze kuangalia vipindi mbalimbali vya kwenye
televisheni.
Popular Posts
-
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Dr Godwin Lekundayo akiwaongoza viongozi wenzake katika maombi wakati wa ugawaji wa...
-
Miongoni mwa changamoto inayoonekana kwa sasa katika teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) ni suala la ulinzi katika mitandao...
-
Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania (BASATA) limetoa siku saba kwa wasanii,vituo vya radio,runinga wamiliki wa tovuti na wa...
-
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam...
-
Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema hajapokea maombi ya Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Ta...
-
Waziri na waziri wa uchukuzi Dr Harrison mwakyembe amesema kuwa Teknolojia ya kisasa inayotumika katika uwanja wa ndege wa kimataifa...
-
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa...
-
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeingilia kati wizi wa fedha kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeibua hofu kubwa katika s...
-
Click the image to open the interactive version (via http://pennystocks.la ).
-
Watumiaji wa simu za Nokia na Windows wamekuwa wakitamani kutumia huduma ya ujumbe wa maneno ya BlackBerry (BBM) huduma hiyo sasa itap...