Serikali ya Tanzania imewatahadharisha wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEKINOHAMA) ili kuondoa vitendo vya uhalifu hapa
nchini.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi Prisca
Ulomi wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam.
Akifafanua Bi Prisca amesema kuwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa kutambua umuhimu wa TEKINOHAMA wameamua kuandaa muswada wa Sheria za Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao (Cyber Laws).
Akieleza
zaidi Bi Prisca amesema kuwa Muswada wa sheria hizo ni pamoja na
Muswada wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi (The Personal Data
Protection Bill), Muswada wa Sheria ya Biashara ya Miamala ya
Kielektroniki (Electronic Transaction Bill), na Muswada wa Sheria ya
Kuzuia Uhalifu kwa njia ya Kompyuta na Mtandao (Computer and Cyber
Crimes Bills).
“Sheria hizo zitasaidia kuimarisha matumizi ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini kwa kudhibiti uhalifu
kwa kutumia mitandao na kuwalinda watoto dhidi ya matumizi yasiyofaa ya
mitandao”. alisema Bi Prisca.
Bi Prisca aliongeza kuwa serikali
imetumia gharama kubwa kuweka miundombinu ya TEHAMA ambayo imesaidia
kuboresha na kuharakisha utoaji wa huduma mbalimbali na kubainisha kuwa
wapo baadhi ya watu wanatumia vibaya teknolojia hiyo, hivyo kuna umuhimu
wa kuwepo sheria zitakazodhibiti uhalifu kupitia mitandao.
Wizara
ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia imetoa rai kwa wananchi
kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao na badala yake watumie vizuri
mitandao hiyo kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla hali inayoweza
kuathiri ukuaji wa sekta hiyo nchini.
Tuesday, April 1, 2014
Popular Posts
-
SERIKALI YA TANZANIA YASEMA:KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAITAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Jana na leo, Serikali ya Tanzania imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunza...
-
Microsoft is switching off its Windows Live Messenger service on 15 March. On that date Messenger log-ins will no longer work a...
-
Watu wengi wameshaona filamu ambazo wahalifu wakidukua simu za mikononi hata kama zimezimwa. Kama ili...
-
Na Yusuph Kileo Nchi ya Tanzania yabahatika tena kwa mara ya tatu kuwa mwenyeji wa mkutano wa “Connect 2 Connect” ambapo kauli mbiu ya...
-
Kutoka Kushoto Gerald Masatu,Mtangazaji Maduhu,Brown Nyanza(IFM),Mama Kagize,Johnson Kuga Mzirai na Jonathan Mnyela Jonathan Mnyela ...
-
Imeelezwa kuwa wananachi wengi bado hawana uelewa wa kutosha juu ya haki zao za msingi katika huduma za mawasiliano wanazotumia, hali ambayo...
-
Wakati bado mafanikio mbali mbali yakijadiliwa wahalifu mtandao wamegundulika kuja na uhalifu unaotafsiriwa kuwa ni wa kihistoria na uliof...