Monday, July 27, 2015

WADUKUZI WADUKUA MAGARI AINA YA JEEP NA KUFANYA YARUDISHWE KWA WAUZAJI

 

Kampuni ya magari ya Fiat Chrysler kutoka Marekani imeyarudisha magari yake yapatayo milioni 1.4 baada ya watafiti wa usalama kuonyesha kuwa magari yao yanaweza kudukuliwa.

Siku ya Jumanne gazeti la teknolojia Wired iliripoti kuwa wadukuzi wamechukua udhibiti wa gari la Jeep Cherokee kupitia mtandao wa mfumo wa burudani.

Chrysler imesema imetoa agizo hilo kwa wamiliki wa magari hayo waliojitolea kuyarudisha.

Kampuni hiyo imesema kuwa udukuzi wa magari yake ni uhalifu.

Watafiti wa usalama Charlie Miller na Chris Valasek walionyesha kuwa wadukuzi hao wanaweza kuyadhibiti magari ya Jeep Cherokee kwa kutumia rimoti, ukitumia mfumo wa burudani wa gari hilo ambalo unashirikiana na mtandao wa simu.

Watafiti hao wawili wa usalama wametumia miaka 5 kuchunguza mifumo ya magari na kubuni mipango ya kuikabili.

Wawili hao wanatarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu kazi yao katika kongamano la Defcon hackers mwezi ujao.

Muda mfupi baada ya tangazo hilo kutolewa ,Bwana Miller aliandika katika akaunti yake ya twitter kuwa anashangazwa na ni kipi nafuu kati ya kutengeza magari salama ama kuyarudisha iwapo kuna tatizo.
Chanzo:BBC

Friday, July 17, 2015

CHUO KIKUU CHA MOUNT KENYA (MKU) CHAANZISHA USAFIRI KWA KUTUMIA BUS LENYE HUDUMA ZA KIDIGITALI






Chuo kikuu cha Mount Kenya (MKU) limeanzisha mpango wa kusafirisha  wanafunzi wa chuo hicho kutumia bus la abiria la kidijitali .
 

Bus hilo lenye viti vya kubeba abiria  62 liloundwa na Kampuni ya  Banbros Ltd ya nchini Kenya linathamani ya shilingi milioni 15 za Kenya likiwa na huduma ya intanet ya wireless ya kasi (Wifi),miundo mbinu ya kupata mawasiliano ya intanet,sehemu za charger ya vifaa vya kiteknohama na televisheni kubwa ambayo inawawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza masomo wakiwa safarini.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Stanley Waudo amesema chuo hicho kimekusudia kutoa elimu bora ya viwango na pia kitahahikisha kina wafikia wanafunzi hata wale ambao wanaweza elimu ya chuo hicho kupitia mtandao.

Friday, July 10, 2015

GHANA YAJIPANGA KUPAMBANA NA UHALIFU MTANDAO

 
Moja ya udhaifu mkubwa unaokumba mataifa mengi hasa barani Afrika ni kutokua na mikakati ya uzuizi endelevu dhidi ya uhalifu mtandao. Imethibitika kuwa nchi nyingi zimekua zikingoja tatizo litokee ndio jitihada zinachukuliwa kutatua tatizo huku athari ikiwa imeshaonekana.

Mwaka huu baada ya Nchi ya Ghana kuwa miongoni mwa waathirika wa uhalifu mtandao ambapo  mtandao mkuu wa serikali ya nchi hiyo inao hudumia tovuti 58 za serikali ulidukuliwa na kusababisha tovuti 11 kuingiliwa na kuathiriwa na wahalifu mtandao; Waziri wa mawasiliano wanchi hiyo Dr. Edward Omane Boamah ametangaza mapambano dhidi ya uhalifu mtandao ili kulinda usalama mtandao wa nchi hiyo.

Tukio hilo la udukuzi  baadae CERT ya nchi hiyo yenye dhamana ya kutambua na  kuzuia uhalifu mtandao kabla haujatokea pamoja na na kuhakiki usalama mtandao wanchi hiyo unaendelea kubeba sura njema ilisema wahalifu mtandao walifanikiwa kudukua tovuti hizo za serikali na kuziathiri vibaya kutokana na mapungufu ya kutokua na program zinazoendana na wakati  katika tuvuti hizo.

Katika hotuba iliyosomwa na Patricia Dovi Sampson kwa niaba ya waziri wa mawasiliano wa Nchi hiyo katika jukwaa la wadau wa maswala ya usalama mitandao Julai Mosi  mwaka huu 2015, iliainisha kua nchi hiyo tayari imetengeneza sera na mkakati wa taifa wa usalama mtandao (National Cyber Security Policy and Strategy (NCSPS) document) ili kupambana na uhalifu mtandao nchini humo.

Ikisisitiza Hotuba hiyo  ilieleza, Nchi hiyo inatambua kuwa uhalifu mtandao hauna mipaka kwani wahalifu udukuzi wa tovuti za serikali ya  nchi hiyo ulionekana wametokea nchini Uturuki. Hivyo ikaelezwa, Nchi hiyo itaimarisha zaidi ufanyaji kazi dhidi ya uhalifu mtandao kwa ushirikiano na mataifa mengine ili kufikia malengo.


Hotuba hiyo pia ilihimiza vyombo vya habari kuongeza jitihada za kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao kwa wanachi wa Nchi hiyo kwani uelewa bado umekua mdogo sana unaosababisha uhalifu mtandao kuzidi kushika kasi nchini humo na kuathiri uchumi kutokana na makampuni ya Kifedha ya Nchi hiyo kuonekana kuathiriwa zaidi.

Aidha, Mshauri mkuu wan chi hiyo katika maswala ya usalama Mtandao Bwana. Albert Atwi-Boasiako, alieleza mafunzo ya uelewa yanayo paswa kufanywa kwa taasisi za serikali na zisizo za serikali bado ya kiwango cha chini sana kwa kiasi kikubwa hali inayo sababisha taasisi hizo kushindwa kuwa na mikakati stahiki na endelevu ya kutambua na kudhibiti uhalifu mtandao kabla haujatokea.

Hivyo mshauri huyo  alitoa Wito kwa taasisi hizo kua na mipango madhubuti ya kujipatia elimu za ufahamu dhidi ya uhalifu mtandao ili kuweza kubaki salama na kupunguza uhalifu mtandao unao kua kwa kasi Duniani kote.

Katika kuhitimisha hotuba ya Waziri wa Mawasiliano Wa Nchi ya Ghana,  wito ulitolewa wa kua na njia rafiki ya ukusanyaji wa taarifa na kupata Takwimu sahihi  zitakazo onyesha kiwango cha uhalifu mtandao huku intelijensia ya utokeaji wa uhalifu huo ikifanyiwa kazi ipasavyo ili kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao nchini humo.

Nini Taifa la TANZANIA linajifunza kutokana na hili?: Ikumbukwe Tanzania pia imekua ni miongoni mwa nchi zilizo ainishwa kua na tabia ya kukabiliana na uhalifu mtandao baada ya kutokea imeaminika njia za kutambua na kudhibiti uhalifu kabla haujatokea bado ni tatizo na jitihada za dhati zina hitajika.

Kwa upande wa Sera na mikakati wa maswala ya usalama mitandao bado taifa Halina kabisa hadi sasa kitu ambacho ni changangamoto kubwa katika kupambana na uhalifu huu mtandao.

Pia Uelewa na nguvu kazi watu imeendelea kua changamoto huku nguvu kazi chache zilizoko kutotumiwa vizuri na taifa. Aidha, ushirikiano kuanzia ngazi ya taifa pamoja na kuvuka mipaka bado umeendelea kua changamoto kubwa inayo paswa kutafutiwa suluhu.

Upambanaji na uhalifu mtandao lazima uwe na mikakati na kuhaki  njia stahiki zilizopendekezwa na wataalam wa usalama mtandao duniani kote zinafatwa ipasavyo ili kuhakiki taifa linabaki salama kimtandao – Bado kumekua na kusua sua kwa kuwekeza katika maswala ya usalama mitandao Nchini huku Taifa kuonekana kupiga hatua kubwa  katika maswala ya TEKINOHAMA ambapo Serikali ya Awamu ya Nne imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwekeza katika Miundo mbinu na ukuzaji wa matumizi ya TEKINOHAMA Nchini.


Ukuaji huu wa kasi wa Miundombinu na utumiaji wa TEKINOHAMA ikumbukwe inaambatana kabisa na ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao Nchini. Hivyo jitihada za dhati na haraka katika kukabilia na Hali tete ya hapo baadae kimttandao zina hitajika hasa Baada ya TANZANIA kuorodheshwa kua ni Nchi ya 6 Inayotegemewa kuathirika zaidi na uhalifu mtandaokatika mwaka wa 2015/2016 huku Ransomeware kwa mara ya kwanza kuonekana kuathiri taifa la Tanzania.

Friday, July 3, 2015

TTCL YAJA NA HUDUMA YA INTANET YA SATELAITI


Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imeendelea kukuza matumizi ya mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) nchini Tanzania  ambapo kupitia kipindi cha msimu wa Sabasaba imeleta teknolojia ambayo itasaidia kampuni, taasisi na ofisi za Serikali ambazo ziko mbali na njia ya Mkongo wa Taifa kupatiwa mawasiliano ya intaneti kwa njia ya satelaiti.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo  jijini Dar es Salaam  kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, katika viwanja vya Sabasaba, Ofisa kutoka TTCL, Fredrick Benard amesema teknolojia hiyo ni muhimu kwa kampuni na kwamba ina ubora, uhakika na kwa bei nafuu.

Benald amesema ili kupata huduma ya intaneti kwa njia ya setelaiti, mteja atapaswa kupeleka maombi rasmi ya huduma anayoitaka na baadaye atapelekewa tathmini ya gharama ya kuunganishiwa.

Aidha amesema, kampuni iliamua kupeleka huduma hiyo kutokana na mahitaji makubwa ya matumizi ya intaneti kwa shughuli za maendeleo.

Popular Posts

Labels