Wabunge wa Tanzania wameibana serikali wakiitaka iboreshe muswada wa sheria ya mifumo ya malipo ili kuzibana kampuni za simu na mabenki,kutokana na kushamiri kwa wizi katika mifumo ya malipo kwa njia ya kielekroniki kwenye simu za kiganjani na miamala ya fedha ya benki.
Wakizungumzia bungeni jana wakati wakichangia muswada huo,wamesema kampuni za simu zinawakata wananchi fedha katika simu zao za kiganjani bila ridhaa yao na hakuna sehemu yoyote wanayoweza kufikisha malalamiko yao ili warejeshewe fedha hizo.
Katika muswada huo uliowasilishwa na Waziri wa Fedha,Saada Mkuya Salum,Serikali imependekeza kuboresha usimamizi na kuongeza udhibiti,kuimarisha mifumo ya malipo,pia kuzuia na kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza katika mifumo hiyo na kuongeza faini kwa kampuni za simu na benki zitakazokiuka sheria na utaratibu.
Popular Posts
-
SERIKALI YA TANZANIA YASEMA:KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAITAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Jana na leo, Serikali ya Tanzania imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunza...
-
Microsoft is switching off its Windows Live Messenger service on 15 March. On that date Messenger log-ins will no longer work a...
-
Watu wengi wameshaona filamu ambazo wahalifu wakidukua simu za mikononi hata kama zimezimwa. Kama ili...
-
Na Yusuph Kileo Nchi ya Tanzania yabahatika tena kwa mara ya tatu kuwa mwenyeji wa mkutano wa “Connect 2 Connect” ambapo kauli mbiu ya...
-
Kutoka Kushoto Gerald Masatu,Mtangazaji Maduhu,Brown Nyanza(IFM),Mama Kagize,Johnson Kuga Mzirai na Jonathan Mnyela Jonathan Mnyela ...
-
Imeelezwa kuwa wananachi wengi bado hawana uelewa wa kutosha juu ya haki zao za msingi katika huduma za mawasiliano wanazotumia, hali ambayo...
-
Wakati bado mafanikio mbali mbali yakijadiliwa wahalifu mtandao wamegundulika kuja na uhalifu unaotafsiriwa kuwa ni wa kihistoria na uliof...