Wednesday, November 9, 2011

MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI YAONGEZEKA TANZANIA


Matumizi ya simu za mkononi yameelezwa kuwa ni mojawapo ya mafanikio ya wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania

Waziri wa wizara hiyo Profesa Makame Mbarawa amesema jijini Dar es salaam jana  kuwa mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa laini za simu kutoka laini 300,000 mwaka 2000 hadi milioni 22 machi mwaka huu.

Profesa Mbarawa alitoa takwimu hizo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru na kueleza mafanikio ya wizara hiyo.

Amesema kutokana na uwekezaji wa sekta binafsi kumejengwa miundombinu mbalimbali kama ya mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unaotarajiwa kuwa na urefu wa km 10,000 baada ya kuzifikia wilaya zote nchini.

Mkongo huo sasa umeunganishwa kwenye mikongo ya majini ambayo kwa sasa imekwisha jengwa kwa urefu wa km 6,700 ambapo km 4,300 zinatumika katika mikoa 19 kati ya 26 iliyolengwa.

Popular Posts

Labels