Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaandaa utaratibu wa kuanzisha mfumo mpya wa kuhama mtandao bila ya kubadili namba ya simu(MNP) na kuhamia mtandao mwingine.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,Prof.John Nkoma anasema mfumo huo utawasaidia watu wote wanaotumia simu nchini humo waliokuwa wanashindwa kuhamia mtandao mwingine kwa hofu ya kubadili namba ya simu,lakini baada ya kuzindua mfumo huu watu watahama mitandao kwa urahisi bila kubadili namba za simu.
Anafafanua kuwa mfumo huo utasaidia kuleta ushindani kwa makampuni ya simu na kuleta faida kwa wateja,pia makampuni hayo yataweza kuongeza ubora wahuduma kwa wateja wao.
TCRA imeandaa makutano wa kimataifa ambao utahudhuriwa na watu zaidi
ya 100 wa kuzungumzia suala hilo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania,Prof.Makame
Mbarawa.
Mkutano huo wa siku mbili unaotarajiwa kuanza kesho
umeandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mawasiliano Duniani (ITU) na
utahudhuriwa na wawakilishi mbalimbali kutoka duniani kote zikiwemo nchi
za Afrika Mashariki
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo aliwataka wananchi kununua vinga'amuzi mapema ili kuondokana na usumbufu ambao unaweza kujitokeza baada ya kuhamia katika mfumo wa digital Disemba 31 mwaka huu.
Popular Posts
-
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Dr Godwin Lekundayo akiwaongoza viongozi wenzake katika maombi wakati wa ugawaji wa...
-
Miongoni mwa changamoto inayoonekana kwa sasa katika teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) ni suala la ulinzi katika mitandao...
-
Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania (BASATA) limetoa siku saba kwa wasanii,vituo vya radio,runinga wamiliki wa tovuti na wa...
-
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam...
-
Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema hajapokea maombi ya Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Ta...
-
Waziri na waziri wa uchukuzi Dr Harrison mwakyembe amesema kuwa Teknolojia ya kisasa inayotumika katika uwanja wa ndege wa kimataifa...
-
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa...
-
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeingilia kati wizi wa fedha kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeibua hofu kubwa katika s...
-
Click the image to open the interactive version (via http://pennystocks.la ).
-
Watumiaji wa simu za Nokia na Windows wamekuwa wakitamani kutumia huduma ya ujumbe wa maneno ya BlackBerry (BBM) huduma hiyo sasa itap...