Nchi ya Kenya imechukua hatua ya kwanza katika ujenzi wa kile kinachotarajiwa utakuwa mradi mkubwa zaidi barani Afrika wa mji wa kiteknolojia (Silicon Valley) au unaotegemea sana vifaa vya electroniki katika kuendeleza teknolojia ya habari na mawasiliano.
Rais Mwai Kibaki alizindua rasmi mradi huo katika eneo la Konza,mtaa mdogo kusini mwa Nairobi,ambako mji huo mpya wa kiteknolojia utajengwa katika muda wa miaka 20 ijayo.Rais Kibaki ambaye alizindua mradi huo muda mfupi kabla ya kuondoka madarakani mwezi machi alieleza mji wa Konza utasaidia kubadili uchumi wa Kenya kwa kiasi kikubwa.
Mradi huu wenye thamani ya Dola bilioni kumi na nne na nusu upo chini ya mpango wa Wizara ya Habari na Mawasiliano.Mradi huo unasemekana kutoa nafasi zaidi ya 100,000 za ajira ifikapo mwaka 2030 pamoja na kuendelea kudumisha ukuaji wa pato la nchi la jumla ya aslimia 10 katika kipindi cha miaka 18 ijayo.
Popular Posts
-
SERIKALI YA TANZANIA YASEMA:KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAITAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Jana na leo, Serikali ya Tanzania imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunza...
-
Facebook wametangaza kitu kipya kwa simu za Android walichokipa jina la Home. Kwa muda mrefu kulikuwa na uvumi kuwa Facebook wana...
-
Microsoft is switching off its Windows Live Messenger service on 15 March. On that date Messenger log-ins will no longer work a...
-
Watu wengi wameshaona filamu ambazo wahalifu wakidukua simu za mikononi hata kama zimezimwa. Kama ili...
-
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dr Ally Simba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevitaka vituo vya redio na televi...
-
Na Yusuph Kileo Nchi ya Tanzania yabahatika tena kwa mara ya tatu kuwa mwenyeji wa mkutano wa “Connect 2 Connect” ambapo kauli mbiu ya...
-
Serikali ya Tanzania inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hivi karibuni kumezuka kundi la Watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakit...