Simu za Android kwa sasa zimekuwa na watumiaji wengi na inawezekana
ndio zinaongoza kwa kuwavutia wezi. Lakini bila kujali kuwa simu yako
imeibiwa au umeisahau sehemu kuna umuhimu wa kuhakikisha unachukua
tahadhari ili inapotokea tukio linalokufanya usijue simu yako iko wapi
uweze kuifatilia. Hizi ni baadhi ya software ambazo unaweza kuweka
kwenye simu yako na kukusaidia pale inapopotea au kuibiwa:
1. Anti Theft Droid
Hii ni App inayokuwezesha kufuatilia simu yako pale inapokuwa
imepotea au kuibiwa. Unapoiweka katika simu yako unakuwa na uwezo wa
kuifuatilia kupitia browser ya internet kama Mozilla au google chrome na
inaweza kukutumia email pale inapotokea simcard ya simu yako
kubadilishwa na kuwekwa nyingine. Pia inakuwezesha kuona picha ambazo
zimepigwa kwenye simu yako pale unapokuwa umeipoteza.
2. Snuko – Android Anti Theft Security
Snuko ni App inayokuwezesha kuifuatilia simu yako ya android kwa
kutumia GPS, Wi-Fi na mnara wa simu inayotumia. Snuko pia inaweza
kuizima simu yako pale unapogundua kuwa imeibiwa na uwezekano wa kuipata
haupo na inaweza kukupa taarifa pale simcard inapobadilishwa.
3. Total Equipment Protection App
Hii inafanya kazi kama nyingine zilizotajwa hapo juu ikikuwezesha
kujua simu yako iko maeneo gani lakini ikiwa na kitu cha ziada ambacho
ni uwezo wa kufuta data zako zote zilizokuwa kwenye simu inapotokea
ukashindwa kuipata simu yako..
4. Cerberus Anti Theft
Cerberus Anti Theft inaweza kutumika kuzilinda simu hadi 5 kwa wakati
mmoja, pia inakutumia taarifa kupitia ujumbe mfupi “SMS”. Kitu kingine
kizuri kuhusu App hii ni kuwa inaweza kufuatilia simu yako iko maeneo
gani kwa kusikiliza mazungumzo kupitia microphone ya simu yako hata kama
alieichukua haitumii kupiga simu.
5. Lost Droid
Lost Droid ni App ambayo inakusaidia kuitafuta simu yako iliyopotea
kwa kutumia computer yako. Inaweza kukutumia taarifa ya mahali simu yako
ilipo kupitia SMS bila kusahau kuizima simu yako kwa kutumia SMS.
Chanzo:tanganyikanblog
Popular Posts
-
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Dr Godwin Lekundayo akiwaongoza viongozi wenzake katika maombi wakati wa ugawaji wa...
-
Miongoni mwa changamoto inayoonekana kwa sasa katika teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) ni suala la ulinzi katika mitandao...
-
Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania (BASATA) limetoa siku saba kwa wasanii,vituo vya radio,runinga wamiliki wa tovuti na wa...
-
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam...
-
Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema hajapokea maombi ya Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Ta...
-
Waziri na waziri wa uchukuzi Dr Harrison mwakyembe amesema kuwa Teknolojia ya kisasa inayotumika katika uwanja wa ndege wa kimataifa...
-
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa...
-
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeingilia kati wizi wa fedha kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeibua hofu kubwa katika s...
-
Click the image to open the interactive version (via http://pennystocks.la ).
-
Watumiaji wa simu za Nokia na Windows wamekuwa wakitamani kutumia huduma ya ujumbe wa maneno ya BlackBerry (BBM) huduma hiyo sasa itap...