Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA Imewataka wananchi wa mikoa ya Tabora na Singida kuepukana na dhana potofu ya matumizi ya televisheni walizonazo kuwa hazitumiki katika matangazo ya kidijiti bali waendelee na televisheni zao kwani king’amuzi hakina luninga maalum.
Hayo yamebainishwa na Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano na Utangazaji nchini Tanzania Bwana Fredrick Ntobi wakati akitoa taarifa ya kuzima mitambo ya analojia ifikapo tarehe 31 machi mwaka huu itakayohusisha maeneo ya mikoa hiyo.
Ntobi amesema kuwa utaratibu wa kuzima mitambo ya analojia utakuwa kwenye mitambo ya maeneo ya dijitali ambapo watoa huduma za kusambaza ving’amuzi walioko Tabora kuhakikisha kuwa kuna ving’amuzi vya kutosha.
Aidha wananchi wa mkoa Tabora wasizitupe tv zao za analojia bali wanunue ving’amuzi ili kupata matangazo ya kidijitali.
Hata hivyo wakizungumza na vyombo vya habari baadhi ya wananchi wa mkoa wa Tabora wameonesha wasiwasi wao kuhusu mfumo mpya wa kidijitali wa upataji wa matangazo ya televisheni kwa kuwa watu wengi bado hawajanunua ving’amuzi na ambao wamenunua wanalamika kuwa baadhi ya chaneli hawazipati.
Thursday, March 27, 2014
Popular Posts
-
anzania imejaaliwa kuwa na kampuni na taasisi kadhaa zinazohusika na mawasiliano na nyingi ni binafsi zinazojiendesha kwa faida kubwa kabisa...
-
SERIKALI YA TANZANIA YASEMA:KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAITAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Jana na leo, Serikali ya Tanzania imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunza...
-
Afisa wa Taasisi ya uwezeshaji na ujengaji uwezo kwa wateknohama nchini KINU, Catherinerose Barretto akimkabidhi cheti Ally Said toka P...
-
Wapiga kura 2,845,256 wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa mwili wa binada...
-
Serikali ya Tanzania inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hivi karibuni kumezuka kundi la Watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakit...
-
Kanisa la River Side lililopo mtaa wa Njiro jijini Arusha, Tanzania, limetangazwa kuwa ni kanisa pekee barani Afrika ambalo limefikia...
-
Lagos, Nigeria - A little over a decade ago there were about 100,000 phone lines in Nigeria, mostly landlines run by the state-owned tel...
-
Watafiti toka kampuni ya utafiti ya Zscalar wamegundua kuwa,tovuti za kichina zenye picha za ngono zimekuwa zikisamb...