Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania limekanusha uvumi wa ujumbe mfupi wa maneno
unaoendelea kusambazwa kwenye simu na mitandao ya kijamii kuhusiana na Papa kumtaka Rais
Barack Obama wa Marekani kupitisha sheria ya kuabudu siku ya jumapili mwezi huu.
Akizungumza katika kipindi cha Kanisani jumahili kupitia Morning Star Radio ambacho huwapatia nafasi Viongozi mbalimbali wa Kanisa hilo kutoa mada na kuulizwa maswali na wasikilizaji Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika Unioni ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji James Machage amesema kuwa ujumbe huo ni uvumi na wa uongo ambao hauhusiana na kanisa hilo,kwani kanisa lina utaratibu maalum wa kutoa matamko yanayolihusu na sio katika ujumbe wa maneno katika simu ama kwenye mitandao ya kijamii.
Toka jumatano iliyopita blog hii imekuwa ikitumiwa na kushuhudia ujumbe huo ambao mwanzoni ulikuwa kwa lugha ya kiingereza na ijumaa ukawa umetafsiriwa kwa lugha ya kiswahili hali ambayo imeleta sintofahamu miongoni mwa waumini wa kanisa la Waadventista Wa Sabato
Ujumbe wenyewe wa kiingereza "Doreen
Emmau: The Pope urging US President Barrack Obama to pass the National
Sunday Law this month,SDA President Ted Wilson is appealing to
all SDA members around the world to pray and have a personal
consecration and revival and reformation of Godliness for 7 days either 7
am or 7 pm for the outcome of the Holy Spirit in the form of the latter
rain.Plse send to all SDA members.Many will be cold in faith,a prophecy
that will go back to the fold of the Beast the pope itself.Be Watchful
my friend,Jesus is at the Door....He is coming be Ready....Harry Coombs"
Wa kiswahili "Papa amwomba rais wa marekani Barack Obama atangaze sheria ya taifa ya
jumapil mwisho wa mwezi huu, rais wa wasabato Ted wilson anawaomba
waadventista wasabato duniani kote kufanya maombi na matengenezo kwa
siku saba kwa ajili ya utauwa wa kweli muda wa maombi ni saa 1 asbh au 1
jioni kwa kumwagwa roho mtakatifu kwa namna ya mvua.Tafadhali tuma sms
kwa waadventista wasabato.Rafiki yangu kesha na uwe tayari YESU anakuja
yuko mlangoni"
Naye Katibu Mkuu wa Konferensi ya Mashariki mwa Tanzania Mchungaji Sadock Butoke amesema jana kuwa kanisa hilo halina taarifa hizo na ujumbe huo unapaswa kupuuzwa.
Saturday, October 18, 2014
Popular Posts
-
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Dr Godwin Lekundayo akiwaongoza viongozi wenzake katika maombi wakati wa ugawaji wa...
-
Miongoni mwa changamoto inayoonekana kwa sasa katika teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) ni suala la ulinzi katika mitandao...
-
Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania (BASATA) limetoa siku saba kwa wasanii,vituo vya radio,runinga wamiliki wa tovuti na wa...
-
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam...
-
Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema hajapokea maombi ya Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Ta...
-
Waziri na waziri wa uchukuzi Dr Harrison mwakyembe amesema kuwa Teknolojia ya kisasa inayotumika katika uwanja wa ndege wa kimataifa...
-
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa...
-
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeingilia kati wizi wa fedha kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeibua hofu kubwa katika s...
-
Click the image to open the interactive version (via http://pennystocks.la ).
-
Watumiaji wa simu za Nokia na Windows wamekuwa wakitamani kutumia huduma ya ujumbe wa maneno ya BlackBerry (BBM) huduma hiyo sasa itap...