Tuesday, December 8, 2015

JWTZ YATOA ONYO KWA WANAOPIGA PICHA NA KUZISAMBAZA KWENYE MITADAO YA KIJAMII


Mkurugenzi wa Habari  na Uhusiano  wa Jeshi la
Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ-Kanali Ngemela Lubingo (Chanzo:Mwananchi)

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa onyo kwa wananchi kutojihusisha na upigaji picha wa vifaa vya kijeshi na kuvisambaza katika mitandao ya kijamii.

Hatua hiyo inakuja kutokana na tukio la  Desemba 3,saa 1:15 jioni ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius JK Nyerere jijini Dar es salaam wafanyakazi wa Shirika la kupokea mizigo la Swiss Port wakishirikiana na wale wa shirika la Ndege la Uholanzi (KLM) kupiga picha vifaa vya kijeshi na kuvisambaza katika mitandao ya kijamii

Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ Kanali Ngemela Lubingo amewaambia Waandishi wa Habari jijini Dar es salaamu kuwa jeshi hilo limesikitishwa na  tukio hilo la watu kujichukulia maamuzi ya kupiga picha kitu ambacho hakikuwahusu na kusambaza picha kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha kujitokeza kwa maoni ya kupotosha jamii


Popular Posts

Labels