Takwimu zilizotolewa na Taasis inayosimamia masuala ya mawasiliano ya Shirika la Umoja wa Mataifa Duniani (ITU)
Februari
,2013 iliyopo Geneva,Uswisi kupitia kituo chache cha kukusanya
takwimu za mawasilliano ya teknolojia ya habari na mawasiliano duniani zinaonesha kuwa watu wanaotumia wa
mawasiliano ya simu wamefikia bilioni 6.8 kati ya watu bilioni 7.1
waliopo duniani.
Takwimu
hizo zinaonesha kuwa matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa
asilimia 96 duniani ambapo asilimia 128 katika nchi zilizoendelea na kwa
nchi zinazoendelea ni asilimia 89.
Kwa
upande wa mawasiliano ya intaneti watu bilioni 2.7 duniani ambao ni
karibia asilimia 40 ndio waliounganishwa katika matumizi ya mawasiliano
hayo ambapo wanawake ni asilimia 16 tu.
Katika
nchi zinazoendelea asilimia 31 wameunganishwa kwenye mitandao ya
komputa ukilinganisha na asilimia 77 ya watu wanaotoka katika nchi
zilizoendelea.Ambapo matumizi ya interneti barani Ulaya ni asilimia 75
na nchi za bara la Amerika ni asilimia 65,wakati barani Afrika ni
asilimia 16 tu.
Takwimu
hizi zinaonesha kuwa kumekuwa na kiwango kikubwa cha matumizi ya
intaneti kwa wanaume kuliko wanawake duniani kwani ni asilimia 37 tu ya
wanawake wanaweza kuwa katika mitandao ambapo wanaume ni asilimia 41.
Katika
nchi zinazoendelea kuna wanawake milioni 826 wanaotumia intaneti na
wanaume ni milioni 980 na katika nchi zilizoendelea wanawake wanaotumia
inteneti ni milioni 475 ambapo wanaume ni milioni 483.Ambapo
inaonekana kuna tofauti ya asilimia 16 kati ya wanaume na wanawake
katika matumizi ya teknolojia hiyo ya mawasiliano katika nchi
zinazoendelea na katika nchi zilizoendelea ni tofauti ya asilimia 2 tu.
Takwimu
hizo pia zinaonesha kuwa inakadiliwa kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka 2013 jumla ya kaya
750 ambazo ni sawa na asilimia 41 duniani ndizo ambazo zitakuwa
zimeunganishwa na mawasiliano ya intaneti.
Popular Posts
-
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Dr Godwin Lekundayo akiwaongoza viongozi wenzake katika maombi wakati wa ugawaji wa...
-
Miongoni mwa changamoto inayoonekana kwa sasa katika teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) ni suala la ulinzi katika mitandao...
-
Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania (BASATA) limetoa siku saba kwa wasanii,vituo vya radio,runinga wamiliki wa tovuti na wa...
-
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam...
-
Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema hajapokea maombi ya Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Ta...
-
Waziri na waziri wa uchukuzi Dr Harrison mwakyembe amesema kuwa Teknolojia ya kisasa inayotumika katika uwanja wa ndege wa kimataifa...
-
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa...
-
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeingilia kati wizi wa fedha kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeibua hofu kubwa katika s...
-
Click the image to open the interactive version (via http://pennystocks.la ).
-
Watumiaji wa simu za Nokia na Windows wamekuwa wakitamani kutumia huduma ya ujumbe wa maneno ya BlackBerry (BBM) huduma hiyo sasa itap...