Serikali ya Tanzania imesema itawachukulia hatua kali za kisheria kwa mtu yeyote atakayebainika kutumia vibaya simu za mikononi na mitandao ya kijamii kuleta uchochezi au kwenda kinyume na maadili ya nchi hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mwishoni mwa juma Waziri wa Sayansi na Teknolojia,Makame Mbarawa amesema lengo la kufanya hivyo ni kukomesha vitendo vya hatarai vinavyoonekana kukua siku hadi siku nchini Tanzania.
Amesema hatua zitachukuliwa dhidi ya kampuni au mtu yeyote atakayetumia njia hizo za mawasiliano kutoa kashfa ama kuitukana serikali,viongozi wa serikali,dini,siasa na watu binafsi kwa kuwa vitendo hivyo vinakiuka sheria za nchini.
Hatua hizo za serikali pia zitawahusu watu wote wanaojihusisha na uonyeshaji kwenye mitandao hiyo picha za ngono,unyanyasaji wa watoto na ukiukwaji wa maadili na kutoa taarifa zenye lengo la kuvunja utulivu na amani.
Teknolojia ya habari na mawasiliano katika miaka ya hivi karibuni imechangia kuleta maendeleo nchini Tanzania lakini baadhi ya watu wanaitumia kwa mambo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na wizi,ujambazi,ubakaji,biashara ya dawa za kulevya, ukahaba na kusambaza siri za watu binafsi bila idhini ya wahusika.
Popular Posts
-
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Dr Godwin Lekundayo akiwaongoza viongozi wenzake katika maombi wakati wa ugawaji wa...
-
Miongoni mwa changamoto inayoonekana kwa sasa katika teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) ni suala la ulinzi katika mitandao...
-
Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania (BASATA) limetoa siku saba kwa wasanii,vituo vya radio,runinga wamiliki wa tovuti na wa...
-
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam...
-
Waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema hajapokea maombi ya Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Ta...
-
Waziri na waziri wa uchukuzi Dr Harrison mwakyembe amesema kuwa Teknolojia ya kisasa inayotumika katika uwanja wa ndege wa kimataifa...
-
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa...
-
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeingilia kati wizi wa fedha kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeibua hofu kubwa katika s...
-
Click the image to open the interactive version (via http://pennystocks.la ).
-
Watumiaji wa simu za Nokia na Windows wamekuwa wakitamani kutumia huduma ya ujumbe wa maneno ya BlackBerry (BBM) huduma hiyo sasa itap...